Mwalimu wapewa onyo kali

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, amesema  Mwalimu Mkuu atakayeruhusu mwanafunzi aliyejifungua kurudi skuli kuendelea na masomo katika skuli za serikali, atafukuzwa kazi.

Aliyasema hayo jana wakati akihutubia wakaazi wa Sengerema katika uzinduzi wa mradi wa maji.

“Ni ukweli pia kuwa wanafunzi waliopata mimba hawarudishwi skuli, kuna ujanja ujanja wa walimu, wanaandikika cheti kuwa amelazwa, nikumuona Mwalimu Mkuu amerudisha mwanafunbzi aliyepata mimba kwenye skuli za serikali ataondoka,” alisema.

“Kwani wote waliopata mimba wamebakwa?, wanafanya mambo haya kwenye picha, wakipata mimba kwa namna hiyo arudi shule,” alihoji.

Aliwataka wazazi kuwachunga watoto kwani mimba hizo zinatokana na wazazi hivyo lazima wajifunze kulea akisema Watanzania wamechagua kueleza ukweli hivyo waambiane ukweli.

Aidha alizitaka asasi za kiraia (NGO’s) zinazotetea wanafunzi hao kufungua skuli zake kama kweli zinawependa.

“Si kwamba nawachukia wenye mimba, hata kama bahati mbaya akapata mimba, kama hizo NGOs zinawatetea sana zifungue skuli za wenye mimba kwa sababu zinawependa,” alisema.

Alisema hata hao wanaofanya makongamano ya kuhamasisha watu wapate mimba wafungue skuli zao kwa ajili ya wanafunzi hao.

“Haiwezekani fedha za walipa kodi shilingi bilioni 17 kila mwezi za kusomeshea watoto wetu kwenda kusomesha akina mama, wazunguke, waimbe, waseme mini ndie Rais huo ndio ukweli,” alisema.

Pia alisema amepata mialiko zaidi ya 60 kwenda nje ya nchi baada ya kuwa Rais lakini ameikataa kwa sababu anataka kuishughulikia Tanzania kwanza.

Alisema hana haja ya kwenda nje ya nchi kwa sababu bado ana mzigo mkubwa wa kumaliza ufisadi.

“Niende nje kufanya nini wakati nitakwenda tu nikishastaafu, nataka nimalize kwanza haya hapa ndani,” alisema.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s