Balozi Seif asifu mchango wa Diaspora

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, alisema serikali inatambua umuhimu wa taasisi zinazoundwa na Watanzania walioko nje (Diaspora) katika kuchangia maendeleo ya uchumi wa Zanzibar.

Alisema hali hiyo imeifanya  serikali kuunda Idara ya Uratibu ya Wazanzibari  wanaoishi nje ya nchi  na ushirikiano wa kimataifa ili kuzipa nguvu taasisi hizo.

Alisema hayo wakati akizungumza na timu ya madaktari, wataalamu wa sekta ya sfya na wauguzi kutoka Marekani wanaounda timu ya Diaspora ambao wapo Zanzibar kutoa huduma za matibabu bure katika hospitali kuu ya Mnazimmoja.

Alisema azma timu hiyo ya madaktari kusogeza huduma za kijamii kwa wananchi imeleta faraja kwa serikali iliyojipanga kuimarisha huduma za afya katika kila masafa yasiyopungua kilomita tano.

“Sera ya afya Zanzibar inaagiza vituo vya afya viwepo kila baada ya kilomita tano ili kuwaondoshea shida ya kupata huduima hiyo wananchi hasa vijijini,” alisema.

Aliwahakikishia madaktari hao chini ya mwamvuli wa diaspora kwamba serikali itaendelea kushirikiana kuhakikisha malengo waliyojipangia yanafanikiwa kwa kiwango kikubwa.

Hata hivyo, aliwaasa wananchama wa jumuiya hiyo na wale wenye asili ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kukunjua zaidi mikono yao katika kusaidia jamii yao ili faida ya uwepo wao nje ya nchi iweze kuonekana zaidi.

Alisema ni vyema masuala hayo yakaenda sambamba kwa wanachama hao kuangalia hatma ya maisha yao ya baadae wakielewa kwamba nyumbani kutabakia muhimu kwao katika maisha yao ya baadae.

Mapema kiongozi wa timu ya madaktari hao, Mtaalamu wa maabara, Asha Nyang’anyi, alisema timu yake imejipanga kutoka huduma za afya kwa wananchi wa rika zote.

Alisema uwepo wao nchini utatoa fursa kwa watu kuchunguzwa afya zao hasa kwa maradi ya ngozi, shindikizo la damu, kisukari na afya ya akina mama.

Alisema uamuzi wao huo umekuja baada ya washirika wa taasisi hiyo kutoka nchi mbali mbali duniani hasa zile za Afrika wanaoishi Marekani kujikusanya pamoja wakilenga kusaidia jamii ya nchi zitakazohitaji huduma za kijamii ambazo ziko ndani ya uwezo wao.

Timu ya wataalamu hao inaundwa na diaspora kutoka Nigeria, Cameroun, Lesotho, Norway, Canada na Tanzania.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s