Chochoro za uuazaji Karafuu kienyeji wabainika

karafuu

MKUU wa wilaya ya Wete, Rashid Hadid Rashid, amesema katika msimu huu wa karafuu atahakikishaa anakabiliana na wananchi wanaofanya biashara haramu ya kununua karafuu mbichi na kavu kinyume na taratibu kwa njia ya kikombe na pishi.

Alisema tayari serikali imeshazibaini chochoro na njia zinazotumiwa na wananchi hao kuendesha biashara hiyo haramu ambapo wamejipanga kuhakikisha biashara hiyo inakomeshwa na karafuu zinauzwa ZSTC.

Akizungumza na wafanyabiashara na wakulima wa karafuu katika jimbo la Mtambwe, aliwataka wananchi kuacha kucheza na serikali badala yake wanapaswa kuheshimu taratibu zilizowekwa ili wasiingie kwenye matatizo.

Alisema mikakati ya serikali ya wilaya ni kuona hakuna hata punje moja ya karafuu ambayo inauzwa kwa wafanyabiashara binafsi.

“Tumeweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha hakuna karafuu ambazo inatoka na kuuzwa kinyume na taratibu; lengo ni kuona karafuu zote zinauzwa kwenye vituo vya ZSTC na sio vyenginevyo,”alisema.

Alisema mikakati mingine iliyoandaliwa ni kudhibiti vitendo vya wizi wa karafuu unaofanywa na wananchi wakati wa uchumaji wa zao hilo.

Naye Mkurugenzi wa Baraza la mji Wete, Philipo Joseph, alisema mfanyabiashara atakaebainika kujihusisha na ununuzi wa karafuu katika duka lake, baraza litachukua hatua ya kumfutia leseni yake kwani atakuwa anaitumia kinyume na sheria.

Mmoja wa wakulima, Mbarouk Saleh, alisema bado sheria zina kasoro na zinaonekana kuwalinda wahalifu kwani watu wanaoendesha vitendo vya hujuma wanashindwa kutiwa hatiani na hivyo kuwafanya waendeleze vitendo hivyo.

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s