Wana Vitongoji washauriwa kusaidia kwao

WAKAAZI wa Vitongoji wilaya ya Chake Chake, wametakiwa kuweka mkazo katika kukiletea maendeleo kijiji chao hasa katika suala la elimu.

Hayo yalielezwa na Ofisa elimu wilaya ya Chake Chake,Harith Bakar Waziri, wakati akichangia katika kikao cha wazazi, walezi, walimu wa skuli, kamati ya sheha na viongozi wa SOS katika kuhamasisha vita dhidi ya udhalilishaji wa watoto.

Alisema wananchi wa Vitongoji wanapaswa kuzinduka kwa kuwekeza kwenye elimu kwa watoto wao  ili waje kusaidia maendeleo ya kijiji chao siku za usoni.

Alisema iwapo wazazi, walezi, watu maarufu na mashekhe, watakuwa tayari kuhamasisha watoto kusoma,vitendo vya udhalilishaji vitapungua.

“Leo muda wa kusoma unawaona watoto wana sahani za samaki, bilingani na biashara nyengine wanauza, hapa kweli tunawekeza katika elimu au biashara,”alisema.

Aidha alisema serikali iko tayari kuwasomesha elimu ya juu watoto wote bure, lakini inakwamwa kutokana na wingi wa wanafunzi wanaohitaji kusoma elimu ya juu.

Mzazi Hamad Abdalla Hamad, alisema wazazi wa Vitongoji wanachangia maovu ya watoto wao, kutokana na kuwakingia vifua wahalifu  wanapofikishwa katika vyombo vya sheria.

Mwalimu Yussuf Ali Abrahman, alisema vitendo vya udhalilishaji na ulawiti kwa watoto vinapotokea vinapaswa kufikishwa katika vyombo vya sheria badala ya kusuluhisha.

Akizungumia elimu alisema, mwamkoa wa elimu umekua mdogo katika shehia hivyo,hivyo wazazi wanapaswa kubadilika ili watoto waweze kwenda skuli kama kawaida.

Vizuri katika suala hilo.

“Katika Mitihani ya majaribio (mock) kwa wanafunzi wa kidato cha pili mwaka huu, kati wanafunzi 315; ni wanafunzi 189 tu ndio waliofanya mitihani hiyo baada ya kulipa ada ya mtihani shilingi 2,000,”alisema.

Raya Said Mbarouk alisema wazazi wako tayari kulea watoto wao, lakini wanakwama kutokana na ugumu wa maisha huku akitolea mfano watoto nane alionao, mmoja yuko chuo kikuu na mmoja yuko kidato cha nne na wote wanahitaji huduma yake.

Sheikh Khamis Suleiman Ali, alisema muitiko ni mdogo kwa wazazi wa Vitongoji katika kujua maendeleo ya watoto wao, jambo ambalo linarudisha nyuma mustakbali mzima wa maisha yao.

Ofisa elimu kutoka SOS Pemba, Gharib Abdalla Hamad, aliiomba jamii ya Vitongoji kuwa mstari wa mbele katika malezi ya watoto wao ili kuwa na jamii iliyostarabika.

Chanzo: Zanzibar Leo

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s