Mabaharia kiungo cha maendeleo

 

SERIKALI imesema imeridhia mikataba ya kimataifa kuhusiana na ajira za mabaharia ili kuhakikisha ajira zao zinaendelea kukua kwa kasi na kukuza uchumi wa nchi.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, alisema hayo katika maadhimisho ya siku ya mabaharia duniani yaliofanyika Rahaleo.

Alisema mabaharia ni kiungo muhimu katika kukuza uchumi wa nchi, hivyo wanapaswa kuthaminiwa na kutambuliwa kipaji chao.

Aidha alisema mwaka 1974 Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania iliamua kujiunga na Shirika la Bahari Duniani (IMO) ambalo lipo chini ya Umoja wa Mataifa kwa lengo la kukuza na kusimamia utendaji wa sekta ya usafiri majini,kusimamia ulinzi na usalama na kuhifadhi mazingira ya bahari.

Alisema inakadiriwa asilimia 90 za biashara za kimataifa duniani zinategemea meli, hivyo mchango wa usafiri wa meli ni mkubwa zaidi ikilinganishwa na njia nyengine za usafirishaji.

“Hii inamaanisha kwamba mabaharia ndio nguzo muhimu katika kubeba, kuangalia, kutunza na kufikisha salama abiria, mizigo na mali zinazosafirishwa duniani kote,” alisema.

Hata hivyo, alisema serikali inatambua changamoto zilizopo ambazo zimesababisha mabaharia nchini kushushwa katika meli za kimataifa na kuchangia kupungua kwa ajira.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Baharini (ZMA) Abdalla Hassan Kombo, alisema kuna nchi mbali mbali   zilizopiga hatua ya maendeleo ya uchumi kupitia mabaharia.

Alisema nchi hizo ni pamoja na Philippines ambapo katika soko la kimataifa mabaharia waliosajiliwa ni 367,166 na kuingiza dola milioni 575.72 nchini mwao kwa mwaka.

“Kwa sasa China inaongoza kwa kutoa mabaharia wengi wakifuatiwa na Philippines na Russia,hata hivyo soko la mabaharia la China linatumika zaidi kwa soko la ndani ikilinganishwa na nchi ya Philippines na Russia,” alisema.

Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, Gilliard Ngewe, alisema dunia ya sasa ni ya sayansi na teknolojia hivyo lazima mabaharia wa Tanzania wajifunze kuingia katika soko la biashara za majini.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s