Wanaodaiwa ZHELB wahimizwa kulipa

BODI ya Mikopo Elimu juu Zanzibar (ZHESLB) imewataka wadaiwa ambao wameshaajiriwa kwenye taasisi za umma na binafsi, kufanya hima kurejesha mikopo hiyo ili kutoa fursa kupatiwa wanafunzi wengine.

Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa bodi hiyo Pemba, Ahmada Omar Juma, wakati akitoa taarifa ya urejeshaji wa mikopo kwa wakopaji kuanzia mwaka 2011 hadi Mei mwaka huu, ofisini kwake Chake Chake.

Alisema inawezeka wakopaji mara baada ya kumaliza masomo hujisahau kwamba fedha hizo zinahitajika kurejeshwa, ili na wengine waombe, hivyo ni vyema wakakumbushwa.

Alisema sio vyema kwa wadaiwa hao kungojea bodi kutumia sheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani, kuwafuatilia wadhamini au waajiri wao, bali wajihimu kurejesha kwa hiari.

Alisema idadi ya wanafunzi wanaopatiwa mikopo inaweza kuongeza Zanzibar kutoka 594 hadi kufikia 1,600, kama kasi ya urejeshaji wa fedha itakuwa nzuri.

Hata hivyo, alisema uombaji wa mikopo kwa mwaka 2017/2018 umeshaanza tokea Mei 2 mwaka huu, na unatarajiwa kumalizika Julai 30 na hadi sasa ni wanafunzi 65 pekee kisiwani Pemba waliojitokeza kuomba.

Aidha aliwaomba wadhamini na waajiri kuendelea kutoa taarifa za uajiri mpya kila wanapoajiri ili bodi hiyo iweze kufuatilia iwapo kuna aliesoma kwa njia ya mkopo.

Chanzo: Zanzibar Leo

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s