Lowassa atakiwa kurudi Julai 13

1

Na Mwandishi wetu

WAZIRI Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chadema, Edward Lowassa, amewasili makao makuu ya polisi jana kama alivyoelekezwa siku ya Jumanne baada ya kuhojiwa kwa saa nne.
Lowassa aliwasili saa 5.52 asubuhi akiwa ameambatana na viongozi wengine wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, huku ulinzi mkali ukiwa umewekwa katika makao makuu hayo.
Mbali na hao walikuwepo watu wengine aliombatana nao, lakini walizuiliwa kuingia na askari walioimarisha ulinzi katika eneo hilo.
Askari hao pia waliwafukuza waandishi wa habari waliokuwa katika eneo hilo na kuwataka kusogea mbali ya viunga vya makao makuu hayo.
Hata hivyo, baada ya muda mfupi Lowassa aliondoka huku Mbowe akieleza kuwa ametakiwa kurudi Julai 13 kwa kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Lowassa alitakiwa kufika polisi jana akikabiliwa na tuhuma za kutoa kauli ya kichochezi wakati wa futari iliyoandaliwa Juni 23 na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.

Katika futari hiyo, Lowassa anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi kuhusu Masheikh wa Taasisi ya Uamsho wanaoshikiliwa akidai utaratibu wa kisheria ufanyike ili kuwaachia huru.
Jumatatu wiki hii Lowassa alipokea wito wa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz, kwenda kuhojiwa juu ya tuhuma hizo na alitakiwa kuripoti saa 4.00 asubuhi siku ya Jumanne.

Aliwasili Jumanne saa 3:58 asubuhi kama alivyotakiwa akiwa na msafara wa gari nne ambazo zilisindikizwa na gari mbili za polisi.
Alihojiwa kwa saa nne mfululizo kabla ya kuachiwa kwa dhamana saa 8.15 mchana na kuelekea nyumbani kwake, Masaki ambako alizungumza na vyombo vya habari.

Baada ya kuachiwa, wakili wake, Peter Kibatala, ambaye pia alikuwepo katika mahojiano hayo,alisema Lowassa amejidhamini mwenyewe na alitakiwa kuripoti tena kwa DCI jana saa sita mchana ili kujua taratibu watakazoambiwa.
Kibatala alisema Lowassa alihojiwa kwa kosa la uchochezi kwa kauli yake aliyoitoa Juni 23 na kwamba baada ya kuhojiwa aliandika maelezo ya onyo juu ya kauli yake ambayo imetafsiriwa kuwa ni ya kichochezi.
Maelezo hayo ya onyo yanaweza kutumika dhidi ya Lowassa kama akifikishwa mahakamani.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s