Kenya yazuia gesi, unga wa Tanzania

103F93BA-8BB9-4344-A6BB-674B7FC3DC9C_cx0_cy8_cw0_w1023_r1_s

SERIKALI imesema Kenya imekataa kuruhusu unga wa ngano kutoka Tanzania kuingia nchini humo bila ya kutozwa ushuru jambo ambalo Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki imelieleza kama ukiukwaji wa taratibu za kibiashara za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Katibu Mkuu Wizara ya Biashara, Prof. Adolf Mkenda katika taarifa yake alisema, kutokana na hilo serikali ya Tanzania nayo imebidi kuchukua hatua madhubuti kwa nia ya kumaliza tatizo hilo, ingawa hakuanisha hatua zilizochukuliwa.

Mbali ya unga, Kenya imepiga marufuku uingizwaji wa gesi ya kupikia (Liquefied Petrolium Gas, LPG) nchini humo kutokea Tanzania na kwamba gesi itakayoruhusiwa kuingia Kenya ni ile itakayokuwa imepitia kwenye bandari ya Mombasa pekee.

Alisema baada ya taarifa hiyo kutolewa Aprili mwaka huu, serikali ya Tanzania iliwasiliana na Kenya ili kupata maelezo kuhusu hatua hiyo ambayo ni kinyume cha taratibu za kibiashara katika Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

Alisema Mei 18, 2017 ya Kenya ilitekeleza uamuzi wake kwa kuzuia shehena ya gesi isiingie Kenya kutokea Tanzania.

Alisema hatua hiyo ina athari kubwa kwa wafanyabiashara wa gesi ya kupikia nchini pamoja na watu wote ambao ajira zao zinategemea biashara hiyo.

Wakati hatua hizo zinachukuliwa bado Kenya ilikuwa haijatoa maelezo rasmi kwa Tanzania kuhusu uamuzi wake huo.

Alisema katika kikao cha Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kilichofanyika Juni 2, 2017, suala la hatua ya Kenya kupiga marufuku uingizwaji wa gesi kutokea Tanzania lilizungumzwa kwa kirefu na kufanyiwa maamuzi.

“Kimsingi serikali ya Kenya ilikubali kuondoa katazo la uingizaji wa gesi kupitia Tanzania mara moja na makubaliano haya yaliingizwa kwenye kumbukumbu za mkutano ambazo ziliafikiwa na nchi zote wanachama wa Jumuiya kwa kuweka saini,” alisema.

Alisema pamoja na makubaliano haya, Kenya imeendelea kuzuia gesi isiingie nchini mwao kutokea Tanzania.

Chanzo: Zanzibar Leo

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s