Viongozi wa serikali wauawa Kibiti

SAUF-2

NA MWANDISHI WETU

VINGOZI wawili wamepigwa risasi katika kijiji cha Mangwi kilichopo kata ya Mchukwi wilayani Kibiti usiku wa kuamkia jana.

Waliopigwa risasi wametajwa kuwa ni Mtendaji wa kijiji hicho, Shamte Makawa na Mwenyekiti wa kitongoji cha Mangwi, Maiko Nicholaus.

Pia wauaji hao walimpiga, Mwenyekiti wa kitongoji cha Londo, Michael Martin risasi ya macho, iliyoharibu macho yake mawili na kuchoma moto nyumba ya Martin na kisha kutokomea kusikojulikana.

Mganga wa zamu katika kituo cha afya Kibiti, Dk. Sadock Bandiko, alithibitisha kuuawa kwa viongozi hao wa kijiji hicho.

Alisema Shamte alikutwa na majeraha matatu yaliyotokana na kupigwa risasi.

Kwa upande wa mwenyekiti wa kijiji hicho, Dk. Sadock alisema marehemu alipigwa risasi moja ya shingoni iliyopigwa kutoka upande wa kulia.

Pia alisema mwenyekiti huyo alikuwa na jeraha kubwa katika mguu wake wa kushoto lililotokana na kukatwa na kitu chenye ncha kali.

Mganga Mkuu wa hospitali ya Mchukwi, Dk. Zacharia Lukeba, alipolazwa Martin, alisema alipigwa risasi moja ya kichwani iliyofumua na kuharibu kabisa macho yake.

Alisema tayari wamempa rufaa kwenda hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Mmoja ya ndugu za marehemu hao, alisema watu wanne waliokuwa na bunduki wakiwa wamevaa nguo nyekundu na kuficha sura zao kwa soksi walivamia kijijini hapo saa 4.00 usiku.

Alisema watu hao walianza kwenda kwa Mwenyekiti wa kijiji hicho, Hamis Bakari Mkima (30) ambaye alifanikiwa kuwakimbia kabla hawajamfikia.

Alisema watu hao walimpiga kwa kitu chenye ncha kali katika mguu wake wa kushoto kisha kumrejesha kwake wakimtaka awapeleke kwa viongozi mbalimbali wa kijiji hicho.

Alieleza baada ya hapo walimtaka awapeleke kwa Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho (Mwarami Shamte) na baada ya kufika huko walimpiga risasi tatu na alifariki dunia papo hapo.

Alisema watu hao pia walimtaka Mwenyekiti huyo awapeleke kwa Mwenyekiti wa kitongoji cha Londo na baada ya kufika kwake walimpiga risasi ya usoni iliyoharibu macho yake.

Alisema baada ya hapo walimpiga risasi moja Mwenyekiti huyo wa kijiji cha Mangwi, (Hamis Mkima) na alifariki papo hapo.

Pia alieleza wakati watu hao wakifanya hayo walikuwa tayari wamechoma moto nyumba ya Mwenyekiti wa kitongoji cha Londo kwa kutumia mafuta ya petroli yaliyokuwemo kwenye pikipiki yake na kuteketeza kabisa nyumba yake yote.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga, amekiri kutokea tukio hilo.

Alisema polisi wamekwenda eneo la tukio kwa ajili ya ufuatiliaji.

Watu 37 wameuawa kwa kupigwa risasi tangu vitendo vya mauaji vilipoanza katika wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji mkoani Pwani Januari 2015 wakiwemo askari polisi 13.

Akizungumzia mauaji hayo, Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, alisema suala la mauaji yanayoendelea katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji, linahitaji mshikamano na kuwa mauaji hayo hayapewi nafasi ya kuendelea.

Zitto aliandika hayo kwenye ukurasa wake wa facebook na twitter na kutaka taifa lizungumze lugha moja ili kukabiliana na mauaji hayo.

“Ninarejea wito nilioutoa siku zilizopita kuwa ninatarajia Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama itakwenda eneo la ‘MKIRU’ kuzungumza na wananchi wa kule ili kupata maarifa ya mbinu za kuishauri na kuisimamia serikali kudhibiti mambo na kuimarisha usalama,” aliandika.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s