Mabodi awakemea waharibifu Pemba

DSC_1721

NAIBU Katibu  Mkuu   wa  CCM Zanzibar,  Dk. Abdulla  Juma  Saadalla (Mabodi) amewasihi  wananchi  wa  shehia ya Ndagoni  mkoa wa Kusini Pemba kulinda miundombinu ya maji safi na salama isiharibiwe na baadhi ya watu wenye tabia  ya kuhujumu  miundombimu hiyo kwa makusudi.

Nasaha hizo alizitoa wakati akikagua  miundombinu ya maji iliyotengenezwa na Mamlaka ya Maji Pemba baada ya kuharibiwa na watu wasiojulikana.

Alisema maji ni muhimu kwa maisha ya kila siku kwa wananchi wote hivyo ni lazima miundombinu yake ithaminiwe na kuwekewa ulinzi wa kudumu.

Aliwambia wananchi hao kuwa siasa za chuki na migogoro zimepitwa na wakati hivyo wabadilike na kuanza kuishi kwa misingi ya umoja na ushirikiano kwa lengo la kuharakisha maendeleo.

Aidha alisema dhamira ya CCM ni kufanya siasa zenye ushindani wa kutatua kero za wananchi ili waweze kupata huduma bora za kijamii.

Alitoa pole kwa wananchi wa Pemba waliothirika na mvua na kusababisha uharibifu wa mali na vifo.

Pamoja na hayo Mabodi alisema mbali na changamoto hizo chama hicho kitaendea   kuishauri serikali itafute ufumbuzi wa kudumu wa kumaliza changamoto za kilimo zinazowakabili wananchi wa jimbo la Ole.

Akizungumza katika ziara hiyo, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Pemba, Omar Mshindo, alisema mamlaka hiyo haitomvulimia mtu yeyote anayefanya vitendo vya uharibifu wa miundombinu ya maji na atakayebainika atachukuliwa hatua za kisheria.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s