Waandishi TBC Zanzibar wavamiwa

images

WATU waliokuwa na silaha za moto, wamevamia gari ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Zanzibar na kupora begi lililokuwa na kamera na vifaa vyengine vya kazi.

Tukio hilo lilitokea juzi mchana katika maeneo ya Benbella wakati waandishi wa habari wa chombo hicho, walipokuwa wakielekea kazini katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Vuga.

Akizungumza na Zanzibar Leo, mpiga picha wa shirika hilo, Mohammed Awadh, alisema wakati wakitoka ofisini zilizopo jengo la bima Mperani, kuelekea ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Vuga,  walipofika maeneo ya barabara ya kuelea Mnazimmoja na Vuga, lilitokea gari ambalo halina namba  kwa nyuma na kuwazingira kwa mbele.

Awadh ambae pia ni dereva wa gari ya shirika hilo, alisema alipoona hivyo aliamua kusimama ndipo watu wawili walishuka kutoka kwenye gari hilo na kuwalazimisha kutoa kila kitu kilichokuwa ndani.

Alisema alijaribu kubishana nao lakini kuona hivyo watu hao walimtolea bastola ndipo alipowaachia na kuondoka nalo.

Alisema gari la watuhumiwa liliondoka kwa kasi kuelekea babara ya Mnazimmoja  hadi Kariakoo.

“Tulijaribu kuwafuata kwa nyuma lakini kwa tahadhari lakini walipofika maeneo ya Kariakoo hatukujua walikoelekea,” alisema.

Alisema inawezekana wahalifu hao walikuwa wakifikiria kuwa begi hilo lilikuwa na fedha hasa kwa kuwa ofisi zao zipo kwenye jengo moja linalotumiwa na benki.

“Inawezekana walitufuata tokea tunatoka ofisini na walipoona tumebeba begi kubwa wakadhania ni pesa hasa kwa sababu tulikuwa tunatoka kwenye jengo ambalo linatumiwa pia na benki,” alisema.

Alisema tukio hilo wameliripoti makao makuu ya polisi Zanzibar, ambako waliahidiwa kushungulikiwa.

Chanzo: Zanzibar Leo

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s