Utafiti wa Ujenzi ufanyike- Balozi

100

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi ameziagiza taasisi zinazosimamia mipango Miji, Mazingira, Ardhi na Halmashauri kukaa pamoja na mjenzi wa jengo la msikiti wa Mitondooni Kisauni, ili kuzitafutia ufumbuzi hitilafu zilizojitokeza katika ujenzi wa masikiti huo.

 

Balozi Seif alitoa agizo hilo jana alipofanya ziara hafla ya kukagua jengo la msikiti linalojengwa katika eneo hilo linalotarajiwa kuwa na madrasa itakayoatoa elimu ya dini.

 

Alisema taasisi hizo ni vyema zihusike katika utafiti wa kina wa michoro ya ujenzi wa masikiti huo na kuridhina nayo kulingana na mazingira ya eneo lenyewe, ili kuendelea na ujenzi na kuepuka athari zinazoweza kujitokeza hapo baadae.

 

Alisema ujenzi wa majengo ya taaluma na ibada yanayozunguuka makaazi ya watu ambayo yako katika maeneo yasiyo ya kawaida kama vile sehemu zinazotuwama maji yanahitaji kufanyiwa utafiti, ili kuepuka athari ambazo zinazoweza kuepukwa.

 

Balozi Seif alieleza kwamba, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar isingependa kushuhudia kujitokeza kwa migongano kati ya wananchi na wafadhili au wadau wanaoamua kusaidia miradi inayotekelezwa kwa faida ya kuinufaisha jamii.

 

Alisisitiza taasisi zilizopewa dhamana ya kusimamia masuala mbalimbali hapa nchini kuhakikisha zinawajibika ipasavyo kwa watendaji kufuatilia na kuifanyia ukaguzi miradi wanayoisimamia.

 

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Idara ya Mipango Miji na Vijiji, Muhammad Juma alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, kwamba Taasisi yake itakuwa tayari kumsaidia mjenzi wa jengo hilo ili azma yake ya kuweka vitenga uchumi vinavyolenga kuuendesha msikiti huo itimie.

 

Muhammad alisema hatua hiyo itachukuliwa kutokana na  hali halisi ya eneo linalojengwa msikiti huo kuwa na kawaida  ya uhifadhi wa maji yanayotoka milimani  wakati wa msimu wa mvua.

 

Hata hivyo, Mkurugenzi huyo alikiri kwamba taasisi yake bado ina ipungufu wa maofisa wanaohusika na ukaguzi na ufuatiliaji wa masuala yanayohusu ujenzi katika maeneo mbalimbali Unguja na Pemba.

 

Ujenzi wa msikiti Mitondooni uliopo Kisauni  kwa mujibu wa michoro, ramani  na mazingira ya eneo hilo unatarajiwa kujengwa kama ulivyojengwa msikiti  mabuluu uliopo Gulioni.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s