Majadiliano mabovu huzaa mikataba ovyo

 

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Shamata Shaame Khamis, amesema suala la kuwa na mikataba yenye tija ni wajibu wa msingi kwa wanaoshiriki kuingia mikataba kwa niaba ya serikali.

 

Imeelezwa kuwa, mara nyingi vyombo vya kutunga sheria ikiwemo Baraza la Wawakilishi na Bunge linapokuja suala la mikataba ya serikali mijadala na hisia nzito hujitokeza kutokana na kile kinachoelezwa baadhi ya mikataba inayofungwa ni mibovu na isiyo na tija.

 

Kauli hiyo aliitoa wakati akifungua mafunzo ya siku tano ya majadiliano na mikataba yaliyowashirikisha wanasheria wa serikali na wajumbe wa Kamati ya Katiba na Sheria ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, yanayofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Unguja.

 

Alibainisha kuwa, mikataba hiyo pia inaonyesha dhahiri kuwa hainufaishi nchi na matokeo yake inatoa fursa kwa upande wa pili wa mikataba kunufaisha zaidi.

 

Aidha, alisema mafunzo hayo yana lengo la kuwapatia ujuzi wa majadiliano ya mikataba, kwani itatoa fursa kwa kuwapatia ujuzi utakaoongeza ufanisi katika suala zima la mikataba.

 

Naibu Shamata, alisema mafunzo ya majadiliano ya mikataba ni muhimu sana ikizingatiwa kuwa majadiliano yanayofikia kwenye makubaliano ndio yanayoweka masharti ya mikataba kwa kupatikana wakati wa majadiliano.

 

Alibainisha kuwa, kazi ya mwandishi wa mikataba ni kuyaweka makubaliano hayo katika mfumo wa mikataba kwani majadiliano mabovu ndio yanayozaa mikataba yenye changamoto na isiyo na tija.

 

Hata hivyo, alisema kimsingi mkataba uliokwisha kutiwa saini masharti yake hayawezi kubadilishwa na upande mmoja tu uliotiwa saini kwani lazima ipatikane ridhaa ya upande wa pili.

 

Hivyo, aliwaomba washiriki wa mafunzo hayo kuyachukua mafunzo watakayopatiwa kwani wana wajibu mkubwa wa kujifunza ili kuhakikisha taifa linafanikiwa kwa mikataba inayoingiwa na serikali.

 

Sambamba na hayo, alibainisha kuwa kuyapuuza mafunzo hayo athari yake inaweza kuleta madhara makubwa kwa nchi ikiwemo kupoteza rasilimali za nchi kutumiwa kwa kunufaisha wachache.

 

Athari nyengine alisema ni kuwepo kwa manung’unuko na migongano kati ya serikali na wananchi pamoja na mataifa ya nje, kutoa mwanya kwa wanasiasa kuishutumu serikali na viongozi kwa kutengeneza matabaka kati ya wanachi na serikali yao pamoja na kuichafua taaluma ya sheria.

 

Mbali na hayo, aliwasisitiza kuthamini juhudi za serikali katika kuwaendeleza kiujuzi ikiwemo kushiriki ipasavyo katika mafunzo hayo na kuongeza ubora katika kazi zao kwa manufaa ya taifa.

 

Nao washiriki wa mafunzo hayo, waliahidi kuyafanyia kazi ili kuongeza uelewa mpana zaidi kuhakikisha mikataba inayosainiwa na serikali inakuwa na ubora kwa maendeleo ya nchi na taifa kwa ujumla.

 

Mafunzo hayo ya siku tano yameandaliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia mradi wa mabadiliko ya sekta ya sheria Zanzibar.

Chanzo: Zanzibar Leo

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s