SMZ kununua mahine ya DNA

index

SERIKALI imesema haioni umuhimu wa kutenga siku ya kupinga vitendo vya udhalilishaji Zanzibar, hasa ikizingatiwa tayari zipo siku maalumu za kimataifa za kuadhimisha siku hiyo.

Miongoni mwa siku hizo ni pamoja na siku ya mtoto wa Afrika, siku ya wanawake duniani na siku 16 za wanaharakati za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud, alisema hayo wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa mfumo wa kisheria unaohusiana na uendeshaji wa kesi za udhalilishaji wa wanawake na watoto.

Aidha alisema serikali kupitia Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto kwa kushirikiana na taasisi nyengine inafanya jitihada za kuelimisha jamii juu ya namna ya kupambana na kuvikomesha vitendo hivyo kupitia vyombo vya habari, mikutano, skuli, mihadhara ya kidini na makongamano.

Alisema katika mwaka wa fedha 2017/2018 serikali imetenga shilingi bilioni moja kwenye fungu la Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kununua mashine ya DNA ili kuwatia mikononi wahusika na shilingi milioni 175 milioni zitakazotumika kwa shughuli za mapambano ya udhalilishaji.

Pia alisema maombi ya ajira za washauri nasaha kwa ajili ya vituo sita vya mkono kwa mkono yamepelekwa Tume ya Utumishi serikalini.

Vile vile katika mwaka ujao wa fedha, alisema serikali imeweka vipaumbele vya kupambana na kukomesha udhalilishaji nchini kwa kuandaa mtandao imara utakaowezeshwa kufanyakazi kwa utaalamu na kwa uhakika saa 24 ili kesi zote zipatiwe ufumbuzi unaostahiki.

Pamoja na hatua hiyo, alisema serikali imeazimia kuweka utaratibu wa kisheria wa kuwachukulia hatua kali wahusika wa kesi hizo ambao watasuluhishana katika ngazi ya kijamii na kufuta kesi hizo.

Mapema wakichangia taarifa hiyo, Wawakilishi walisema ipo haja ya kuanza kuchukuliwa hatua viongozi wote wa serikali watakaosaidia kusuluhisha kesi za udhalilishaji.

Mwakilishi wa jimbo la Tungu, Simai Mohammed Said, alisema alisema kufanya hivyo ni kutasaidia kudhibiti udhalilishaji na wimbi la viongozi wanaotumia nafasi zao kuzifanyia suluhu kesi hizo.

Nae Mwakilishi wa jimbo la Chake Chake, Suleiman Sarahani, alisema upo umuhimu wa kuangalia kwa makini chanzo cha vitendo hivyo.

Alisema ufuatiliaji huo ufike hadi vijijini pamoja na kuweka mtandao wa kuwafichua wanaowafanyia vitendo watoto vitendo hivyo.

Mwanasha Khamis Juma mwakilishi wa jimbo la Chukwani, akizungumzia mashine za DNA, alisema ununuzi wa kifaa hicho utakuwa mkombozi kwa wanawake na watoto.

Chanzo: Zanzibar Leo

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s