Makungu awaonya Majaji, Mahakimu

unnamed (28)

 

JAJI Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu, amewataka Majaji, Mahakimu na Makadhi, kufuata maadili ya kazi na kuacha kujiingiza katika vitendo vya rushwa ili kulinda heshima ya kazi yao na kujijengea uaminifu kwa wananchi.

 

Hayo aliyasema mahakama kuu Vuga, wakati akifungua semina ya siku moja kwa watendaji wa Idara ya mahakama, iliyoandaliwa na Jumuiya ya Majaji, Mahakimu na Makadhi Zanzibar (ZAJOA).

 

Alisema jitihada zaidi zinapaswa kuongezwa hasa katika eneo la uandishi wa hukumu ili kupunguza malalamiko kutoka kwa wenye kesi na wadau wengine wakiwemo wananchi kama si kuyaondoa kabisa.

 

Alisema ingawa hukumu zinatolewa kwa wingi, lakini bado haziridhishi kutokana na watendaji hao kutofuata taratibu za kisheria zilizowekwa huku wengine wakishindwa kuanisha sababu nzuri ya kufikia uamuzi huo.

 

Aidha alisema suala la uandishi wa hukumu ni muhimu kwa watendaji hao kwani amebaini kesi nyingi zimekuwa zikirejeshwa na kuanza kuamuliwa upya kwa makosa ambayo yapo katika uwezo wa watendaji hao.

 

“Hakuna sheria moja ya uandishi wa hukumu; kila mmoja anaweza kuandika kwa mtindo wake muhimu mambo muhimu yanatakiwa yazingatiwe”, alisema.

 

Alisema wenye kesi na wasikilizaji wanachohitaji kujua ni mgogoro unahusiana na nini,ushahidi gani umetolewa na upande husika na kwa kiasi gani  umefanyiwa tathmini ya kutosha na Jaji, Hakimu au Kadhi kabla ya kufikia kutoa hukumu.

 

Nae Naibu Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo Luciano Makoye Nyengo alisema mafunzo hayo ni endelevu na hivi karibuni yatafanyika kwa upande wa wanachama wanaofanya kazi Pemba.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s