Sirro awataka polisi Z’bar kufanya kazi kwa weledi

Kamishna

MKUU wa jeshi la polisi nchini (IGP), Simon Sirro, amewataka maofisa na askari wa jeshi la polisi Zanzibar kufanya kazi kwa weledi, heshima na upendo miongoni mwao ili kutekeleza vyema majukumu yao ya kila siku.

 

Sirro alitoa wito huo makao makuu ya polisi Zanzibar Ziwani, katika ziara yake ya siku moja ya kujitambulisha tokea alipoteuliwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli kushika wadhifa huo.

 

Alisema kwa kuwa wamekula viapo ni vyema watekeleze majukumu yao kwa mujibu wa sheria za nchi, kanuni na miongozo ya jeshi la polisi (PGO) ili wananchi wawe na imani na jeshi lao.

 

“Tuithamini kazi yetu kwa kufuata sheria za kazi kwa kuwa kazi ndio kigezo cha utu na ustawi wa maisha yetu, maisha yetu yote tuliyonayo na heshima yetu inatokana na kazi ya jeshi la polisi hivyo tuwatumikie wananchi kwa sheria bila ya uonevu na upendeleo,” alisema.

 

Aliwataka watekeleze majukumu yao kwa kujiamini bila ya woga na kuwa wakakamavu ili kuondokana na hali ya ulegelege kwa kuwa kazi ya kupambana na uhalifu inahitaji ujasiri mkubwa.

 

“Askari lazima ajue mafunzo yote ya kijeshi na uwezo wa kutumia silaha, hali hii itatufanya tuwe wakakamavu na kuwa tayari kupambana na uhalifu wa aina mbali mbali, tumeona yalitokea Kibiti mkoani Pwani, njia pekee ya kukabiliana nayo ni mazoezi ya kila mara,” alisema.

 

Aidha aliwatanabahisha wale wote wenye mtindo wa kuvujisha siri za jeshi kwa wahalifu na watu wengine waache mara moja na vyenginevyo watachukuliwa hatua kali za kinidhamu ili kukomesha hali hiyo.

 

Hata hivyo, aliwapongeza maofisa na askari hao kwa kudumisha amani na kuahidi kuzipatia ufumbuzi changamoto zote walizoziainisha ikiwemo stahiki zao, maslahi, rasilimali vifaa na upandishwaji vyeo ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kwa ufanisi.

 

Mapema Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame, alimpongeza IGP Sirro kwa ziara yake ya kujitambulisha pamoja na kuzungumza na maofisa na askari hao ili kujua changamoto zinazowakabili.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s