Maalim Seif awapa moyo wafanyabiashara

IMG_7012

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad jana usiku umewatembelea wafanyabiashara wa Zanzibar na kusikiliza maoni yao juu ya hali ya biashara inavyokwenda katika kipndi hiki cha kuelekea Skukuu ya Eid El Fitri.

Katika ziara yake ya ghafla aliyoifanya usiku wa jana Maalim Seif alianzia Maduka ya Mlandege hadi Darajani ambapo alijionea biashara inavyokwenda na kupata nafasi ya kuzungumza na wafanyabiashara hao wa nguo ambapo walimlalamikiwa kwamba hali ya biashara sio nzuri katika kipindi hiki.

Aidha wafanyabiashara hao wamesema kodi zinazotozwa ni nyingi na hali ya biashara hairidhishi kutokana na fedha kutokuwa na thamani lakini wananchi wanashindwa kumudu kununua nguo kutokana na hali ngumu ya maisha ilivyo hivi sasa.

“Kwa kweli hali ya bishara sio nzuri na kila siku tunajitia moyo kuwa kesho biashara itakuwa nzuri lakini kila Ramadhani inapofikia mwisho ndio watu wanazidi kupungua na wengi wanakuja hapa kufanya window shop tu hakuna anayenunua chochote” alisema Mmoja wa wafanyabishara hao.

Naye Bi Nassra Suleiman alimwambia Maalim Seif kwamba wanaipenda Zanzibar na wangependa wabaki kufanya bishara Zanzibar na ndio maana bado wapo hawajaondoka kwenda hata hapo Dar es salaam lakini utitiri wa kodi umekuwa mkubwa na unawavunja moyo wafanyabiashara.

Ali Issa ni miongoni mwa wafanyabiashara amemwambia Maalim Seif kwamba tatizo kubwa ambalo linawakabili ni wingi kodi ambao huwafanya wafanyabiashara kutoweza kuendelea na biashara na kufunga maduka yao.

“Tatizo kubwa Serikali haina mipango na haina nia ya kuwalinda na kuwasaidia wafanyabiashara na ndio maana wengi wetu wanaishia njiani katika kufanya biashara” alieleza Issa.

Akizungumza na wafanyabiashara hao Maalim Seif aliwataka wafanyabiashara hao kuwa na subra na kuendelea kuwapatia huduma wateja wao kama kawaida licha ya hali ngumu inayowakabili.

Alisema kawaida kwa Serikali zisizo na ridhaa ya watu kujikusanyia makodi ambayo hayana tija kwa wananchi kwani kodi hizo haziwanufaishi wananchi wala nchi enyewe.

Amewataka wafanyabiashara hao kutovunjika moyo kwani yeye mwenyewe anajua namna hali ilivyokuwa ngumu na wafanyabiashara hao walivyokuwa na changamoto kubwa ya kodi pamoja na hali ya kutokuwepo biashara.

“Tunajua kama mnakabiliwa na hali ngumu za kutokuwepo biashara lakini suala la utitiri wa kodi najua hilo linawaumiza wafanyabiashara wengi sana hadi kufika wengine kufunga maduka, lakini Mwenyeenzi Mungu yupo na nyinyi na msivunjike moyo.

Maalim alisema jambo zuri na la kupendeza ni kwamba wafanyabiashara wengi ni wazalendo na wanaipenda sana Zanzibar na ndio maana licha ya changamoto zilizopo bado wanaendelea kulipa kodi na kufanya bishara hapa hapa Zanzibar ili kuisaidia nchi yao. lakini jambo linalovunja moyo Serikali inashindwa kusikiliza kilio cha wafanyabiashara hao.

Maalim Seif amekuwa na kawaida ya kuwatembelea wafanyabiashara  wa nguo na kupita kwenye masoko mbali mbali kusikiliza shida zao kila ifikapo mwezi mtukufu wa Ramadhani na kukaribia Skukuu.

Katika ziara yake hiyo aliyoifanya saa 3 usiku hadi sasa 5 Maalim Seif alifuatana na Naibu Katibu Mkuu Nassor Ahmed, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma, Salim Bimani na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Mashirikiano ya Kimataifa Ismail Jussa.

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s