Dk. Shein: Polisi simamieni amani

2-140

Awataka wapunguze ajali

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, amelipongeza jeshi la polisi Tanzania, kwa kuendelea kusimamia vyema amani na utulivu Zanzibar.

 

Aliyasema hayo jana wakati alipofanya mazungumzo na Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Tanzania (IGP) Simon Sirro, aliyefika Ikulu mjini Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha.

 

Alimueleza IGP Sirro kuwa jeshi la polisi limekuwa likifanya kazi kubwa kuhakikisha amani na utulivu inaimarishwa na wananchi wanajishughulisha na shughuli zao za kijamii wakiwa salama.

 

Alisema jeshi la polisi Zanzibar limekuwa likitekeleza vyema kazi zake na kutoa ushirikiano mzuri kwa wananchi na kusisitiza kuwa ipo haja ya kuongeza ari hiyo ili liweze kuitumikia vyema jamii.

 

Aidha, alieleza imani yake na matumaini makubwa kwa uongozi wa IGP Sirro na kumuahidi kuwa ataendelea kutoa ushirikiano wake ili jeshi hilo lizidi kupata maendeleo na kusimamia amani na utulivu.

 

Alimueleza haja ya kuwepo ushirikiano wa kutosha kwa askari wa barabarani pamoja na taasisi husika inayotoa leseni za udereva wa vyombo vya moto ili kuepusha ajali zisizo za lazima ambazo zimekuwa zikitokezea mara kwa mara.

 

Alisema kumekuwepo ongezeko kubwa la ajaili za barabarani ambazo nyingi husababisha vifo, ulemavu na hasara nyengine za mali, hivyo kuna haja ya kuchukuliwa hatua za makusudi kulitafutia ufumbuzi suala hilo.

 

Dk. Shein alimueleza IGP Sirro haja ya kuitafutia ufumbuzi changamoto ya makaazi inayolikabili jeshi hilo la polisi kwa askari wake waliopo Zanzibar ili kuondokana na hali ya kuishi uraiani.

 

Alitumia fursa hiyo kutoa pongezi zake za dhati kwa Sirro kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo.

 

Nae IGP Sirro alitoa shukurani kwa Dk. Shein na kupongeza kwa ushirikiano mkubwa inaolipata jeshi hilo kutoka kwa wananchi na viongozi wote wa serikali.

 

Alitumia fursa hiyo kuwapongeza wananchi wa Zanzibar kwa kuendeleza amani na utulivu walionao na kusisitiza haja ya kudumishwa na kuimarishwa zaidi kwa maslahi ya nchi na wananchi wake.

 

Alimuhakikishia Dk. Shein kuwa hatua za makusudi zitachukuliwa kuhakikisha changamoto zilizopo kwa jeshi la polisi p Zanzibar zinapatiwa ufumbuzi sambamba na kuahidi kusimamiwa vyema suala zima la usalama wa barabarani.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s