Z’bar lazima iwe na ulinzi wa uhakika

069(1)
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (kulia),akizungumza na Kamanda wa Brigedia Nyuki Zanzibar, Brigedia Jenerali Fadhil Nondo aliyekwenda Ofisini Vuga kujitambulisha.

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, amesema Zanzibar na Tanzania kwa ujumla lazima ziendelee kubakia salama muda wote ili kuwapa fursa wananchi na wageni wanaoingia nchini kufanya mambo yao bila ya bugdha.

Alisema hayo wakati akizungumza na Kamanda mpya wa Brigedia ya Nyuki Zanzibar, Brigedia Jenerali, Fadhil Nondo, aliyefika ofisini kwake kujitambulisha baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.

Brigedia Jenerali Nondo alikuwa akikaimu nafasi hiyo tokea Januari mwaka huu, baada ya aliyekuwa akishikilia wadhifa huo, Brigedia Jenerali Cyrill Ivor Mhaiki, kufariki.

Alisema Zanzibar inapaswa kuwa katika ulinzi wa uhakika muda wote kutokana na mazingira yake yaliyozungukwa na bahari ambayo wakati kwengine hutoa nafasi kwa wahalifu kufanya vitendo vinavyosababisha hofu kwa wananchi.

Alimuhakikishia Kamanda huyo kwamba serikali na viongozi wake iko tayari kutoa ushirikiano ili kuhakikisha anatekeleza vyema dhamana aliyokabidhiwa na taifa.

Alimshauri kushirikiana na makamanda na walinzi wa vikosi vyengine vilivyopo Zanzibar ili kazi yao ya ulinzi ifanyike bila vikwazo.

Mapema Brigedia Jenerali Nondo alimuahidi Balozi Seif kwamba yuko tayari kupokea maagizo yoyote atakayopewa.

Alisema kwa mujibu wa mfumo na taratibu za jeshi,  nafasi yake ya kazi inawajibika kutekelezwa kwa kupokea maagizo na ushauri kutoka kwa viongozi wa juu wa eneo analofanyia kazi.

Kabla ya uteuzi huo, alikuwa Ofisa mafunzo na operesheni wa Brigedia Nyuki na Mkuu wa kambi la JWTZ Bavuai.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s