Ahadi za ‘Sport 55’ zaanza kutekelezwa

DSC_0006

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Riziki Pembe Juma akipokea hundi ya shilingi milioni 5, kutoka Mhasibu Mkuu wa Kampuni ya Samos LTD kupitia hoteli yake ya Karafuu. Mkami Nyamhanga ikiwa ni ahadi ya kampuni hiyo ya kuchangia programu ya ‘Sport 55’.

WADAU mbali mbali wameanza kutimiza ahadi zao walizoziweka katika kuchangia programu ya kuibua na kuendeleza vipaji vya michezo maskulini ‘Sport 55’,baada ya kampuni ya Samos LTD kupitia hoteli yake ya Karafuu kutoa kitata cha shilingi milioni 5.

Hafla ya kukabidhi fedha hizo ilifanyika baina ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Riziki Pembe Juma, na kampuni hiyo iliwakilishwa na mhasibu wake mkuu Mkami Nyamhanga  huko ofisini kwa Waziri Mazizini.

Akizungumza mara baada ya kupokea hundi hiyo Waziri Pembe ameishukuru kampuni hiyo kwa uzalendo wake ulioonyesha kwa kutimiza ahadi walioiweka pasina kukumbushwa.

‘’Nawashukuru sana kwa hiki mlichokifanya, mmeonyesha uzalendo mkubwa sana sio wengi ambao wanatimiza ahadi kama mlivyofanya, nawaomba muendelee na moyo huo katika kusaidia mambo mengine’’alisema.

Alisema kuwa mchango huo utasaidia kwa kiasi kikubwa lengo la kufanikisha mpango huo, ambao ni muhimu sana katika kuleta maendeleo ya michezo ikiwa ndio dhamira kubwa ya Serikali hivi kuona michezo inapiga hatua kubwa kwa kuibuliwa vipaji na kuendelezwa.

Aidha aliahidi kuwa fedha hizo zitatumika kama ilivyokusudiwa kwa faida ya nchi, na kuitaka kampuni hiyo kuendelea kusaidia shughuli mbali mbali za maendeleo katika nchi.

Kwa upande wake mwakilishi wa kampuni hiyo, alisema kuwa kampuni yake itaendelea kusaidia shughuli mbali mbali za michezo na maendeleo ya jamii, ili mafanikio zaidi yaweze kupatikana kwa kuona wananchi wananufaika kwenye nyanja mbali mbali.

Wakati huo huo kampuni ya Zanzibar Cable imetekeleza ahadi yake kwa kutoa shilingi milioni 4.

Mkurugenzi wa Idara ya Michezo na Utamaduni Hassan Khairalla Tawakal, aliwaka wale wpte ambao badpo hawajatekeleza hadi zao, kutekeleza haraka iwezekanavyo ili sema kuwa a

Mei 20 mwaka huu Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, aliongeza harambee ya kuchangia programu ya kuibua na kuendeleza vipaji vya michezo maskulini ‘Sport 55’ ambapo makampuni na watu mbali mbali waliahidi kutoa michango yao.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s