Waliomjeruhi ‘mwizi’ kwa msumeno wa moto wapata dhamana

JALADA la kesi ya watuhumiwa sita wakiwemo wawili wa familia moja wanaodaiwa kumjeruhi, Mahmud Mjengo Ali (28) wakidai kuwa mwizi wa nazi, limepelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) wakisubiri kufikishwa mahakamani.

Watuhumiwa hao kwa pamoja katika kijiji cha Ubago wilaya ya kati Unguja, walimjeruhi mlalamikaji baada ya kumkamata akiiba nazi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Juma  Sadi,  aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Nassor Mohamed Salum (43), Sudi Mohamed Salum (32) na Mohamed Salum Muhsin, wakaazi wa Kidimni na wengine watatu majina yao hayajapatikana.

Alisema watuhumiwa hao baada ya kumkamata mlalamikaji akiwa juu ya mnazi, walimuomba ashuke lakini kutokana na kuhofia usalama wake, hakufanya hivyo.

Alisema baada ya kuona hashuki, ndipo walipoamua kwenda kuchukua msumeno wa moto na kuukata mnazi huo ambao wakati ukianguka ulikwama kwenye mshelisheli pamoja na mlalamikaji.

Alisema baada ya kumuona hashuki, walitumia msumeno kuungusha chini mshelisheli na baada ya mlalamikaji kuanguka walimkata makalio, mguu na mkono na baadae kumtelekeza.

Alisema watuhumiwa hao walipewa dhamana jana lakini wametakiwa kuripoti polisi kila siku hadi kesi yao itakapofikishwa mahakamani.

Akizungumzia matukio mengine, alisema makosa 143 ya aina mbali mbali yameripotiwa kituo cha polisi Tunguu mkoa wa Kusini Unguja, kwa kipindi cha wiki moja iliyopita, ikiwemo la ubakaji.

Alisema kati ya makosa hayo, 136 yanahusu usalama barabarani, shambulio la aibu kosa moja, kuumiza mwili moja, wizi makosa mawili na kesi tatu za kupatikana na gongo na dawa za kulevya.

Alisema mtuhumiwa aliekamatwa kwa kosa la kubaka ni Mustafa Juma Haji (38) mkaazi wa Kizimkazi Dimbani wilaya ya kusini Unguja.

Alisema mtuhumiwa huyo alimbaka msichana (15) mkaazi wa Kizimkazi Dimbani, ambaye yupo chini ya uangalizi wa wazazi wake.

“Vitendo vya udhalilishaji na shambulio la aibu vinazidi kuongezeka kila kukicha, lakini nitahakikisha ndani ya mkoa wangu likitokezea sitolifumbia macho, vitendo hivi vinarejesha nyuma maendeleo ya wanawake,” alisema.

Aidha alisema, katika kijiji cha Dunga Kinyongo, wahalifu wasiojulikana waliiba mbuzi watatu wenye thamani ya shillingi 210,000 mali ya Maabadi Mohamed Khamis (70).

Pia alisema mtuhumiwa Tatu Khamis Juma (22) mkaazi wa Ukongoroni alikamatwa kwa tuhuma za kuunguza nyumba ya aliekuwa mume wake kutokana na wivu wa mapenzi.

Chanzo: Zanzibar Leo

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s