JUMAZA yatoa tamko kutukanwa kwa Mtume Muhammad Salla Allaahu Alayhi wa Sallam

dkt-abdallah-saleh

Kwa kumbukumbu zilizopo hii si mara ya kwanza kwa kijana Abdalla kutoa matusi, kashfa na kufru kwa Allaah, Mtume Salla Allaahu Alayhi wa Sallam na Uislamu kwa jumla. Madaktari na wafanyakazi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja ambapo kijana huyo anafanya kazi…

TAMKO LA JUMUIYA YA MAIMAMU ZANZIBAR (JUMAZA) KWA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU KADHIA YA DK. ABDALLA SALEH ABDALLA KUMKUFURU ALLAAH NA KUMTUKANA NA KUMDHALILISHA MTUME WETU MUHAMMAD SALLA ALLAAHU ALAYHI WA SALLAM TAREHE 28/12/2016
Kamati Tendaji ya JUMAZA ilikaa katika kikao chake cha dharura tarehe 27 Disemba, 2016 kujadili na kutafakari video iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii ikimuonesha Dk. Abdalla Saleh akimkufuru Allaah (S.W) pamoja na kumtukana matusi makubwa sana mpaka ya nguoni na kumdhalilisha Mtume wetu Mtukufu kipenzi cha umma Muhammad Salla Allaahu Alayhi wa Sallam. Baada ya kujadili kwa undani JUMAZA inatamka ifuatavyo:-
1. Kwa taarifa ambazo JUMAZA imezipata Dk. Abdalla Saleh Abdalla anatoka katika familia ya Kiislamu huko Wete Pemba lakini aliamua kurtadi muda mrefu sasa wakati akiwa nje ya Zanzibar.
2. Kwa kumbukumbu zilizopo hii si mara ya kwanza kwa kijana Abdalla kutoa matusi, kashfa na kufru kwa Allaah, Mtume Salla Allaahu Alayhi wa Sallam na Uislamu kwa jumla. Madaktari na wafanyakazi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja ambapo kijana huyo anafanya kazi walishamuonya mara kadhaa kuhusu tabia yake hiyo. Hata hivyo, huwa hasikii, hupuuza na kufanya kibri. Hivyo ni wazi kuwa vitendo anavyofanya anafanya makusudi kwa malengo anayoyajua yeye mwenyewe.
3. JUMAZA, Waislamu wa Zanzibar pamoja na Waislamu wa Dunia kwa ujumla hawako tayari kuvumilia hata kidogo kitendo cha kumtukana na kumdhalilisha Mtume wao Salla Allaahu Alayhi wa Sallam kama alivyofanya kijana Abdalla. Aidha, aelewe kijana huyu Waislamu wako tayari wakati wowote kujitoa muhanga kama ilivyotokea katika historia ya Maswahaba Watukufu ili kulinda hadhi na heshima ya Mtume wao Salla Allaahu Alayhi wa Sallam.
4. JUMAZA inaungana na Mufti wa Zanzibar na Waislamu wote kulaani kwa nguvu zake zote kitendo hiki cha uchochezi na kuiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kumkamata haraka, kumdhibiti na kumchukulia hatua za kisheria. JUMAZA inatoa ushauri huu kwa nia njema ili kulinda amani ya nchi na utulivu na hasa kwa kuzingatia kuwa raia wake wengi ni Waislamu wanaoumwa sana na Dini yao.
5. JUMAZA inaungana na Mufti wa Zanzibar kuvitaka vyombo vinavyohusika kumchukulia hatua mara moja kijana Abdalla, kumfungulia mashtaka na kumpandisha mahakamani ili sheria ifuate mkondo wake. Hii ni kwasababu sisi tunaamini kuwa kitendo alichokifanya kijana Abdalla kinakiuka moja kwa moja Sheria za Zanzibar.
6. JUMAZA na Waislamu wote wana imani kuwa hukumu ya kiuadalifu itatolewa kwa kijana huyu ili Waislamu waendelee kuwa na imani na viongozi wao na Serikali yao kwa ujumla. Aidha, JUMAZA inaonya kuwa hatua yoyote ya kudharau kuchukua hatua kali dhidi ya kijana Abdalla inaweza kupelekea matokeo ambayo si mazuri  katika nchi yetu. Hivyo, kuwajibika ipasavyo kwa vyombo vinavyohusika ndio njia pekee ya kuepusha uwezekano wa Waislamu kuchukua hatua mikononi mwao.
7. JUMAZA inakumbusha tena kuwa kosa alilolifanya kijana Abdalla tena kwa makusudi na kibri ni kosa zito sana na hukumu yake katika Sheria za Kiislamu kama alivyosema Mufti ni kukatwa kichwa. Hatahivyo, kwa kuwa Zanzibar haifuati Sheria za Kiislamu basi itumie sheria zake za kiserikali dhidi ya kijana huyu ili kulinda heshima yake kama nchi inayojali utawala bora pamoja na kulinda heshima kwa Dini zote.
8. JUMAZA inawaomba Waislamu wote kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu na kuvipa nafasi vyombo vinavyohusika kuchukua hatua zake dhidi ya kijana Abdalla. Hata hivyo, inawaomba Waislamu kulifuatilia suala hili kwa karibu zaidi ili kujua hatma yake.
9. Mola wetu Mtukufu tunakuomba uinusuru Dini yako na Waislamu kwa jumla dhidi ya maadui wa ndani na nje. Amiin.
Ahsanteni
Muhiddin Zubeir Muhiddin
KATIBU MTENDAJI
JUMAZA
ZANZIBAR
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s