Msimamo wetu kwa Zanzibar haujabadilika – Balozi Katarina

Balozi Katarina Rangnitt (kushoto) akiwa pamoja na Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein
Balozi Katarina Rangnitt (kushoto) akiwa pamoja na Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein

Balozi wa Sweden nchini, Katarina Rangnitt amesema msimamo wa nchi yake kuhusu suala la Zanzibar haujabadilika na pia ameishauri Serikali kukubaliana na mkataba wa Makubaliano ya Ushirikiano wa Kiuchumi (EPA) baina ya nchi za Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya (EU).

Balozi huyo pia ametahadharisha kuwa udhibiti wa safari za nje ukizidi unaweza kuikosesha nchi fursa huku akishauri vyama vya siasa kushiriki kikamilifu kwenye mjadala wa mustakabali wa Taifa.

Balozi Rangnitt alisema hayo katika mahojiano maalum na gazeti la Mwananchi yaliyofanyika ofisini kwake.

Akizungumzia suala la Zanzibar, Balozi Rangnitt alisema Sweden itasimamia tamko la awali lililotolewa na umoja wa ulaya la kuzitaka pande zinazokinzana kukaa chini na kusaka suluhu ya amani itakayomaliza mzozo wa kisiasa visiwani humo.

EU, ambayo ilikuwa imetuma waangalizi wake ilitoa tamko ikisema kuwa uchaguzi ulifanyika kwa amani na utulivu na kusema kuwa Jecha hakuonyesha uthibitisho wa uamuzi wake wa kufuta matokeo na kwamba kwa wakati wote alikuwa haonekani.

EU haikutuma wawakilishi wake kuangalia marudio ya uchaguzi ulioanyika Machi 20 ambao ulisusiwa na CUF ikisema uamuzi wa kurudia haukuwa shirikishi wala jumuishi. Kutokana na CUF kususia, CCM ilipata ushindi wa viti vyote vya uwakilishi na urais.

Tangu wakati huo, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad,ambaye aligombea urais na ambaye anadai alishinda, amekuwa akizunguka sehemu mbalimbali dumani kuelezea hali ya kisiasa.

Chanzo – Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s