Achomwa kisu nje ya kituo cha polisi Pemba

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu

MTU mmoja Massoud Amour Seif (54) mkaazi wa Mtambile wilaya ya Mkoani Pemba, amefariki dunia baada ya kudaiwa kuchomwa kisu nje ya kituo cha Polisi cha Mtambile na ndugu yake wa damu, Kassim Amour Seif (43), baada ya kutokea ugomvi wa wake zao.

Taarifa zinaeleza kuwa, wawili hao kabla ya mkasa huo, walianza wake zao kugombana na kisha ugomvi huo kuhamia baina yao, na kupelekea marehemu kabla ya kufariki kupata majeraha na kupewa fomu ya PF3 kwa ajili ya matibabu.

Imefahamika kuwa, baada ya kupata matibabu na kisha kwenda kituo cha Polisi kwa ajili ya maelezo ya kina, marehemu akiwa sambamba na mdogo wake, kisha walitakiwa warejee siku ya pili yake, na kujitokeza mkasa huo.

Mashuhuda wa tukio hilo wanaeleza kuwa, hatua chache kutoka kilipo kituo hicho cha Polisi, ndipo Kassim alipomrukia kaka yake na kumchoma kisu na kupoteza damu nyingi.

“Wakati Polisi wanamshughulika marehemu kwa tukio hilo, mpigaji kisu alichukua gari na kukimbilia eneo la barabara ya Wambaa, na majeruhi akafia njiani akipelekwa hospitali”, alisema shuhuda huyo.

Aidha shuhuda Khamis Haji Omar, alisema tokea asubuhi ya tukio hilo, ugomvi wa wawili hao ulishaanza kwa muda mrefu, ikidaiwa kusababishwa na watoto wao kuibiana simu.

Nae shuhuda Mohamed Ali, alieleza kuwa baada ya kutokea kwa hali hiyo, iliyosababishwa na ugomvi wa watoto wao, ndipo wake zao nao walipoanza kutofahamiana na kisha kuhamia kwa ndugu hao.

Kamanda wa Polisi mkoa wa kusini Pemba, Sheihan Mohamed Sheihan alisema, kwa sasa wanaendelea kumsaka mtuhumiwa huyo Kassim Amour Seif, na akipatikana atafikishwa mahakamani.

Alisema, kwa vile mtuhumiwa huyo baada ya kufanya tukio hilo alikimbia akitumia gari yenye namba za usajili Z 242 HI na kuelekea Wambaa, jeshi lake lilivamia huko na baada ya kuona gari la polisi, mtuhumiwa aliamua kulitelekeza gari lake.

“Mtuhumiwa gari lake aliliawacha na kukimbilia msituni, lakini sisi jeshi la polisi gari tunalo ambalo alilitumia Kassim, na sasa tumeshaweka mitego kila kona na akipatikana atajibu hoja’’,alifafanua.

Hata hivyo Kamanda huyo wa polisi mkoani humo, amesema kwa sasa wanamshikilia kijana Mohamed Ali, ambae alikamatwa na pikipiki ikiwa na damu, akidaiwa kumsafirisha mtuhumiwa.
“Huyu kijana tunae na tunamuhoji, na tuna mashaka nae kuwa ndie aliyemsafirisha Kassim, ili kujihifadhi na hasa baada ya kulitekeleza gari lake, ili kuwakimbia polisi’’,alifafanua.

Tukio hilo lilitokea Disemba mosi majira ya saa kumi na mbili unusu nje ya kituo cha Polisi cha Mtambile wilaya ya Mkoani mkoa wa Kusini Pemba, na likiwa ni la kwanza katika miaka ya hivi karibuni kuwahi kutokea.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s