Balozi Iddi aipiga jeki Taasisi ya Siti Bint Saad

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kulia akimkabidhi mchango wa shilingi Milioni tatu Msaidizi Katibu wa Taasisi ya  Kumbu kumbu ya Siti Binti Saad Bwana Mohammed Suleiman Omar hapo Ofisini kwake ndani ya Jengo la Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kulia akimkabidhi mchango wa shilingi Milioni tatu Msaidizi Katibu wa Taasisi ya Kumbu kumbu ya Siti Binti Saad Bwana Mohammed Suleiman Omar hapo Ofisini kwake ndani ya Jengo la Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  alisema Visiwa vya Zanzibar  vitaendelea kupata heshima Kimataifa kadri siku zinavyoaidi kuyoyoma katika Nyanja ya sanaa na utamaduni kufuatia kazi kubwa iliyokuwa ikifanywa  na Msanii mkongwe wa Visiwa hivi marehemu Siti Binti Saad.

Alisema Mchango wa Siti Binti Saad enzi zake kupitia Taarab asilia umeweza kuleta faraja kwa wapenzi wa Muziki huo katika kudumisha Utamaduni wa Kiafrika ndani ya Mwambao wa Afrika Mashariki, Nchi za Ghuba pamoja na baadhi ya Mataifa ya Bara la Asia.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa nasaha hizo wakati wa kukabidhi mchango wa shilingi Milioni 3,000,000/- alizoahidi kutoa wakati wa hafla maalum ya kuichangia Taasisi ya Kumbukumbu ya Siti Binti Saad iliyofanyika kwenye Hoteli ya Park Hyatt Mjini Zanzibar miezi miwili iliyopita ambapo mgeni Rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein.

Alisema jitihada zilizochukuliwa na Taasisi ya Kumbu kumbu ya Siti Binti Saad ya katika azma ya kutaka kumuenzi mwanamuziki huyo nguli Afrika Mashairiki na Bara la Asia inafaa kuungwa mkono na wapenzi wote wa fani hiyo iwe ndani au nje ya Nchi.

Akipokea mchango huo wa Balozi Seif  Msaidizi Katibu wa Taasisi ya Kumbu kumbu ya Siti Binti Saad Bwana Mohammed Suleiman Omar alimshukuru kiongozi huyo kwa kutekeleza ahadi aliyotoa kiasi kwamba imeleta faraja kwa uongozi wa taasisi hiyo.

Bwana Mohammed alisema katika kuthamini michango ya watoa ahadi  taasisi hiyo imeamua kutoa cheti maalum kwa wachangiaji hao ili iwe kumbu kumbu nzuri kwao na vizazi vyao kutokana na kuunga mkono jambo hilo muhimu.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s