Mamia wafanyiwa uchunguzi wa saratani ya matiti Zanzibar

Mkurugenzi wa Ilala Afya Centre ya Dar es Salaam Jaffer Dharsee (kulia) akibadilishana mawazo na viongozi wa Jumuiya ya watu wanaoishi na saratani Zanzibar  (ZCA) ambapo taasisi hizo mbili kwa kushirikiana na Wizara ya Afya zimeandaa kampeni hiyo

Na Ramadhani Ali

Zaidi ya wanawake 500 wamefanyiwa uchunguzi wa saratani ya matiti, ulioandaliwa kwa ushirikiano wa Jumuiya ya watu wanaoishi na saratani Zanzibar (ZCA), Ilala Afya Centre ya Dar es Salaam na Wizara ya Afya ya Zanzibar.

Kampeni hiyo ya siku moja iliyofanyika Hospitali kuu ya Mnazi Mmoja iliwashirikisha akinamama wenye umri  kuanzia miaka 25 na ilikuwa na lengo la kuweza kuwagundua mapema akinamama wenye tatizo la maradhi hayo ambayo dalili zake zinachelewa kujitokeza.

Daktari bingwa wa uchunguzi wa maradhi ya saratani Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa ZCA Dkt. Msafiri Marijani amesema kampeni hiyo ilihusisha uchunguzi wa “Utrasound”na uchunguzi wa sindano na waliopatikana na dalili watafanyiwa vipimo ili kujua kama ni saratani ama matatizo mengine.

Dkt. Marijani amekumbusha kuwa saratani hadi hivi sasa haina tiba na kitu muhimu ni kuigundua mapema ili kuidhibiti kabla haijaleta athari kubwa hivyo amewashauri wananchi kupima afya zao mara kwa mara.

“Saratani ni maradhi yanayouwa watu wengi duniani kutokana na kuchelewa kugundulika mapema, kitu muhimu ni wananchi kujenga utamaduni wa kuchunguza afya zao,” alisisiti Dkt. Marijani.

Amesema Hosipitali zote za wilaya na vituo vingi vya afya vya vijijini vinatoa huduma ya uchunguzi wa saratani hivyo amewashauri wananchi kuvitumia.

Kiongozi wa Jumuiya ya watu wanaoishi na maradhi ya saratani Zanzibar  Bi. Zakia Mohammed amesema kufuatia uchunguzi huo ambapo zaidi ya wanawake 100 wamebainika kuwa na dalili za saratani, wamegundua kuwa tatizo ni kubwa  kinyume na walivyo fikiria awali.

Amesema kutokana na hali hiyo ZCA itafikiria kununua chombo maalumu cha uchunguzi ‘mamography’ ambacho kinauwezo wa kugundua dalili za awali kabisa za maradhi hayo.

Ameongeza kuwa Jumuiya imeazimia kufanya uchunguzi mwengine wa saratani ya shingo ya kizazi na saratani ya tenzi dume katika siku zijazo kwa vile ni miongoni mwa maradhi yanayowasumbuwa wananchi wengi wa Zanzibar.

Baadhi ya akinamama waliofika Hospitali ya Mnazimmoja kufanyiwa uchunguzi wa saratani ya matiti wakipata maelekezo kutoka kwa mhudumu wa hospitali hiyo
Baadhi ya akinamama waliofika Hospitali ya Mnazimmoja kufanyiwa uchunguzi wa saratani ya matiti wakipata maelekezo kutoka kwa mhudumu wa hospitali hiyo
Mkurugenzi wa Ilala Afya Centre ya Dar es Salaam Jaffer Dharsee akitoa maelekezo kwa akinamama waliofanyiwa uchunguzi wa saratani ya matiti katika kampeni iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa kituo hicho, Wizara ya Afya na ZCA

Chanzo: Maelezo, Zanzibar

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s