Waliokopa elimu ya juu Zanzibar kitanzini

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma alipokuwa akitembelea maktaba ya Wilaya ya Wete Pemba wakati wa ziara yake Kisiwani humo hivi karibuni
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma alipokuwa akitembelea maktaba ya Wilaya ya Wete Pemba wakati wa ziara yake Kisiwani humo hivi karibuni
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imeagiza kwa wahitimu wote wenye mikopo ya elimu ya juu ambao wamekopeshwa na mfuko wa elimu ya juu na bodi ya mikopo wajitokeze kwa hiari zao ndani ya siku 60 kuanzia leo kwenda kuhakiki madeni yao na kutambulisha ajira zao.

 
Hatua hiyo ya kutolewa agizo hilo imekuja baada ya kuwepo mrundikano mkubwa wa wanafunzi waliokopeshwa ambao wanadaiwa fedha hizo na hawajalipa.
 
Waziri wa Wizara hiyo Riziki Pembe Juma alisema hayo alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali na wafanyakazi wa bodi hiyo Ofisini kwake Mazizini.
 
Alisema kutokana na kuweo wadaiwa wengi ambao wamekoeshwa na bodi hiyo na hawajalipa fedha hizo imewabidi kuchukua hatua hiyo.
 
Waziri huyo alifahamisha kuwa kunawahitimu 3,700 ambao wamemaliza miaka ya nyuma 2006 ambao hwajaanza kulipa ni vyema kutafutwa ndani ya mwaka huu wanaanza kulipa fedha wanazodaiwa.
 
Alisema kwa yeyote ambae atakaidi agizo hilo na kwenda kinyume na agizo hilo la ndani ya siku 60 ambae atakwenda baada ya siku hizo au atatafutwa na Serikali basi atalazimika kulipa deni lake analodaiwa na faini kama adhabu ya shilingi 50,000 kwa kila mkato.
 
Waziri huyo alifahamisha kwamba kiwango hicho cha adhabu hatoi yeye kama Waziri bali agizo hilo tayari limetolewa katika sheria namba 3 ya mwaka 2011 ya bodi ya mikopo elimu ya juu.
 
“Hii sheria ipo wazi inawataka wale wote ambao hawajarejesha mikopo hiyo basi wafuate agizo hilo kama wataenda kinyume basi sheria hiyo itafuatwa mimi kubwa ninachokifanya ni kuhimiza utekelezaji wa sheria hiyo isimamiwe ipasavyo na tuondoe muhali ili wanaodaiwa walipe,”alisema.
 
Sambamba na hayo Waziri huyo aliitaka bodi hiyo kufanya nguvu za makusudi kuwasaka wale wote ambao walikopa na kuwa tayari kulipa fedha hizo kupitia taasisi zao za serikali na binafsi ikiwa hadi sasa bado hawajarejesha fedha hizo hadi hivi sasa.
 
“Ikiwa wapo waliokopa lakini hawapo hapa nchini lakini wadhamini wao wapo ni vyema kuwahimiza au waende hao wadhamini wakawahakiki wateja wao ili kuweza kufanya makato ikiwa mdhamini hajaenda ukifuatwa kwa nguvu za serikali basi utazilipa wewe,”alisema.
 
Waziri huyo alitumia muda huo kuita bodi hiyo kushirikiana na Idara ya Utumishi ya Serikali ya Mungano ili kuwatambua wajiriwa wao ambao wanahusika na madeni hayo ili waweze kupatikana na kukatwa fedha hizo kwa urahisi.
 
Akiwataja wahitimu wengine Waziri huyo alisema wapo wahitimu 1,146 waliopatiwa mikopo na waliomaliza vyuo vya elimu ya juu 2015/2016 kwa wale ambao tayari wameshaajiriwa ni vyema kujiandaa kulipa madeni hayo na waliokuwa hawajaajiriwa wanapewa mwaka mmoja kuanza kulipa madeni yao wao wenyewe au wadhamini wao.
 
Mbali na hayo Waziri huyo alitumia muda huo kuitaka Bodi hiyo kuwa wabunifu na kutafuta njia za kupa fedha ili kukuza mfuko huo ili kuweza kuwapatia wanafunzi wengi mikopo hiyo.
 
Alisema ili taasisi iweze kufanyakazi ni vyema kushirikiana kwa watendaji wa taasisi hiyo pamoja na kutatua changamoto ziliyopo kwani kwamujibu wa fedha ziliyopo hazitoshelezi kuwapatia vijana wengi wa elimu ya juu.
 
Hata hivyo alitumia muda huo kuitaka bodi hiyo kutoa mkopo kwamujibu wa vipaumbele vilivyowekwa na serikali na kwa wanafunzi wenyesifa zinazotakiwa.
 
Nae Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu Iddi Khamis Haji alisema wanavyuo karibu ya sabini viliyopo ndani ya nchi na nje ya anchi ambavyotayari wamefunga navyomkataba kwaajili ya kuwasomesha wanafunzi wao.
 
Alisema ndani ya kipindi cha miaka 10 kuanzia 2006 hadi 2016 serikali imetowa Bilioni 34 kwa wanafunzi 4,846 kwa ajili ya kuwakopesha wananfunzi kati ya hizo zilizolipwa si zaidi ya shilingi 1.7 bilioni ndani ya kipindi cha miaka mitatu ambapo sawa na asilimia tano.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s