Polisi na Magereza wakumbushwa kuheshimu haki za binaadamu

Jaji mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu (wa pili kulia) akifuatana na maafisa ya jeshi la Magereza huko Kisiwani Pemba
Jaji mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu (wa pili kulia) akifuatana na maafisa ya jeshi la Magereza huko Kisiwani Pemba
MAOFISA wa Jeshi la Polisi na Magereza nchini wametakiwa kuhakikisha wanazingatia na kuifuata taratibu na miongozo ya kimataifa ya haki za binaadamu, wakati wanapotekeleza jukumu la kuwakamata na kuwaweka kizuizini watuhumiwa wa uhalifu.

 
Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu alipokuwa akifungua kongamano lililojadili uzingatiaji wa haki za binaadamu kwa maofisa wa polisi na magereza ambalo limetokana na azimio la haki za binaadamu la mjini Luanda.
 
Alisema kuzingatiwa kwa mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu, kutawezesha kutoa huduma bora zinazozingatia utu wa bindaamu na kulindwa kwa heshima yake kabla ya kufikishwa mahakamani.
 
Jaji Makungu alisema vikosi vya kulinda sheria nchini Tanzania vimekuwa vikabiliwa na changamoto kadhaa za matukio ya uvunjaji wa haki za binaadamu wakati wanapowatia mbaroni watuhumiwa na wakiwa kizuizini.
 
Alizitaja changamoto hizo ni pamoja na kuwepo madai ya utesaji wa watuhumiwa, kutopatiwa huduma za matibabu, kuwatia nguvuni na kuwaweka kizuizini bila ya kufuata sheria, matumizi ya nguvu za ziada dhidi na kubambikizia kesi.
 
Aidha alisema pamoja na kuwepo mkataba wa nchi za Afrika wa kulinda haki ya mtu na heshima yake anapokamatwa kwa makosa ya jinai ikiwemo kupewa fursa ya dhamana, lakini mara kadhaa huwekwa vizingiti vingi ambavyo husababishwa mtuhumiwa kukosa haki ya dhamana na hatimae kuongeza wimbi la watuhumiwa katika nyumba za mahabusu.
 
Alisema mafunzo hayo kwa kiasi kikubwa yatawawezesha maofisa wa polisi na magereza kuzingatia misingi ya haki za binaadamu wakati wanapotekeelza majukumu yao.
“Mbali ya kuweza kupata taaluma ya utekelezaji bora wa maofisa hawa, lakini pia mafunzo yatawezesha kuwepo matandao baina yao na wadau mbalimbali ambao utawezesha kubadilisha mawazo”,alisema Jaji Makungu.
 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binaadamu nchini Tanzania, Tom Bahame Nyanduga alisema kwa mujibu wa utafiri uliofanywa na CHRAGG umebaini kuwepo kwa uvunjifu wa haki za binaadamu unaofnywa na jeshi la polisi nchini Tanzania.
 
Alisema katika vituo 225 vya polisi vilivyo fanyiwa na utauchunguzi imebainika kuwa udogo wa vyumba vya mahabusu, vyumba hivyo kuwa na mwanga hafifu, ukosefu wa maji ya kunywa huku pi wakitumia mitondoo.
 
Alisema kwa mujibu wa katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 ni marufuku watuhumiwa kuteswa ana kwamba mtesaji anafanya kosa la jinai anapotekeleza mambo hayo.
 
Hata hivyo alibainisha kuwa CHRAGG imebaini vunjwaji wa haki za binadam kwa watuhumiwa ikiwemo wengine kuuawa wakiwa kizuizini kutokana na mateso makali.
 
Mwenyekiti huyo alisema kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi, kuna kiasi cha wahabusu 17,224 wanaosubiri hukumu, huku kiasi cha asilimia 50 wafungwa nao wanasubiri hukumu zao mahakamani.
 
“Tanzania ina tatuzo kubwa la mahabusu, hali inayotokana na kuchelewa kuendeshwa kwa kesi zao mahakamani na wengine wakisikitika kubambikiziwa kesi”,alisema Nyanduga.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s