Kikwete kafanya Mapinduzi Baridi- Maalim Seif


Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad

Asema amefanya mapinduzi baridi. Aliliamrisha Jeshi kuizingira bwawani.
Asema CCM wamesema kua hawatatoa nchi kwa vikaratasi vya kura.

Maalim katika muendelezo wa ziara yake leo amekua akifanya mahojiano katika kipindi cha Voice of Amerika VOA.

Katika kuelezea kile kilichompeleka America Maalim alisema ameenda kwa ajili ya kesi yao ambayo amesema ni kesa ya uchaguzi ambao Jecha Salim Jecha aliufuta kinyume na katiba na kinyume na sheria ya uchaguzi.

Maalim katika kipindi hicho alisema JK alifanya mapinduzi baridi kwa kuliamrisha jeshi kuja kuyapindua maamuzi ya Wazanzibari.

Maalim amesema pia kua alifanya jitihada kubwa kutafta suluhu na viongozi hao na alibainisha kua alikutana na JK lakini JK akamwambia Maalim kua CCM wanakuogopa wanasema utavunja Muungano.

Maalim aliendelea kusema kua jitihada alizozifanya kwa JK pia alizifanya kwa Magufuli na alikutana nae pamoja na makamo wake Samia Suluh Hassan lakini Maalim alishangaa kuskia Magufuli akisema kua hawezi kuyaingilia mambo ya Zanzibar zaidi ya kuleta Jeshi.

Maalim anasema CCM hawako tayari kuachia madaraka kwa kile wanachodai kua wanalinda mapinduzi lakini alisema 2008 walifanya jitihada kubwa na raisi Karume mpaka kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s