Maalim Seif awasili Washington DC


Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad, pamoja na Mhe Jussa waliopowasili, kwenye uwanja wa kimataifa Dulles Airport, Jijini Washington DC, siku ya Jumamosi June 11, kwaajili ya ziara ya kikazi itakayochukua siku 14 nchini Marekani pamoja na Canada.

Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amewasili Washington DC amefuatana na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa CUF, Ismail Jussa, na Katibu wake ambaye pia ni Mkuu wa Watumishi katika Ofisi ya Katibu Mkuu, Issa Kheir Hussein.

Katika ziara hiyo, Maalim Seif na ujumbe wake watashiriki katika vikao na mikutano maalum na pia kufanya mazungumzo na viongozi na maofisa wa Serikali za Marekani na Canada, Wabunge wa nchi hizo, taasisi (think tanks) zinazoshauri sera za mambo ya nje za nchi hizo, taasisi za fedha, taasisi na jumuiya zinazohusika na masuala ya demokrasia na haki za binadamu pamoja na vyombo vya habari.

Mbali na mikutano hiyo ya kikazi, Maalim Seif na ujumbe wake pia watakutana na kuzungumza na Watanzania wanaoishi nchi jijini Washington DC na vitongoji vyake.

Akizungumzia ziara hiyo wakati anaondoka akiwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, mjini Dar es Salaam, Maalim Seif alisema: “Tumewaambia Wazanzibari kuwa ni lazima tuidai haki yao ya maamuzi ya kidemokrasia waliyoyafanya tarehe 25 Oktoba, 2015 kupitia kura zao.

 Maalim Seif Sharif Hamad akiwa katika mapokezi
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s