SMZ yajipanga kutangaza utalii Zanzibar duniani

Wakuu wa Idara za Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo wakifuatilia michango ya wizara yao
Wakuu wa Idara za Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo wakifuatilia michango ya wizara yao

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imesema imeweka mikakati ya kuvitangaza visiwa hivyo katika sekta ya utalii duniani kwa kushiriki kwenye maonyesho ya kimataifa yanayofanyika nchi mbalimbali duniani.

Akijibu hoja mbalimbali za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliochangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Waziri Rashid Ali Juma, alisema sekta ya utalii ndiyo tegemeo la kuingiza mapato ya nchi kwa hiyo serikali imeweka kipaumbele katika kuitangaza sekta hiyo na kutafuta masoko mapya ya utalii.

Alisema kuitangaza sekta ya utalii kunakwenda sambamba na watendaji wa Kamisheni ya Utalii kuhudhuria maonyesho ya kimataifa yanayofanyika katika nchi mbalimbali duniani.

Aidha, alisema uamuzi wa Serikali ya Zanzibar kufungua ofisi ndogo ya utalii Mumbai nchini India, kwa kiasi kikubwa itasaidia kuitangaza sekta hiyo.

Alisema mikakati ya Kamisheni ya Utalii ya Zanzibar kuingia katika masoko mapya ya utalii katika Bara la Asia na Russia ambalo soko lake ni kubwa.

‘Serikali ya Zanzibar imejikita katika kuitangaza sekta ya utalii na kuingia katika masomo mapya katika Bara la Asia na Russia,” alisema.

Wajumbe wa baraza hilo la wawakilishi walipitisha na kuidhinisha Sh. 16,281,900,000 kwa mwaka wa fedha 2016/2017 kwa ajili ya wizara hiyo.

Kati ya kiasi hicho cha fedha, Sh. 9,684,400,000 kwa matumizi ya kawaida na Sh. 6,597,500,000 kwa shughuli za maendeleo.

Chanzo: Nipashe

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s