Vikosi vya SMZ lawamani

Mwakilishi wa Jimbo la Chaani Zanzibar Mhe Nadir Abdul-latif Yussuf (Jussab) akila kiapo cha Utii cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati wa zoezi hilo la kuapishwa Wajumbe wapya wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar
Mwakilishi wa Jimbo la Chaani Zanzibar Mhe Nadir Abdul-latif Yussuf (Jussab) akila kiapo cha Utii cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati wa zoezi hilo la kuapishwa Wajumbe wapya wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar

Baadhi ya askari wa vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), wakiwamo wa Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) wamedaiwa kuwatesa raia na kuwapora fedha wanapokuwa doria katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Mji wa Zanzibar.

Hayo yalisemwa na Mwakilishi wa Jimbo la Chaani, Nadir Abdul¬latif Yussuf, wakati alipokuwa akichangia makadirio na matumizi ya Bajeti ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Vikosi vya SMZ) ya mwaka wa fedha 2016/2017.

Alisema askari hao wameacha kufanya kazi yao ya kuimarisha doria na kuwahakikishia usalama raia na mali zao na badala yake wamekuwa wakikamata vyombo vya moto na kuwapekua mifukoni wahusika kabla ya kuwanyaganya fedha.

“Mheshimiwa Spika, askari wa vikosi vya SMZ wamekuwa wakipiga watu, wanapekua mifukoni na kuchukua fedha. Hata mdogo wangu kafanyiwa kitendo kama hicho na kesi ipo katika kKtuo cha Polisi Madema,” alisema mwakilishi huyo huku ukumbi wa Baraza ukiwa kimya wakati akichangia.

Alisema kuwa vitendo hivyo vinafanywa na askari wachache na kuwaharibia wakubwa wao ambao wamekuwa wakitekeleza majukumu yao kwa uadilifu mkubwa visiwani humo.

Alisema kuwa yeye binafsi alikamatwa na askari hao na kutakiwa kujieleza kwa nini amepita katika sehemu wasiyoruhusiwa kupita watu kwa miguu na kutishiwa kumwagiwa maji na pia kupewa adhabu ya kugalagala chini.

Alisema baada ya kuwajengea hoja nzito, walishindwa kumpatia adhabu hiyo baada ya kufahamu wanazungumza na nani na kumwachia kuendelea na safari yake.

“Mheshimiwa Spika, wafahamishwe nidham ya kazi, wasifanye kazi kwa kunyanyasa watu pamoja na kuwanyag’anya vitu,” alisema Mwakilishi huyo.

Nadir alisema vitendo wanavyofanya baadhi ya askari hao vinakwenda kinyume cha misingi ya utawala wa sheria na kutaka serikali kukomesha vitendo vya askari kupora fedha wakijifanya wapo katika doria.

Hata hivyo, Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Rashid Makame Shamsi alisema kuwa askari wa Vyuo vya mafunzo Zanzibar (Magereza) wanaishi katika mazingira magumu kutokana na nyumba wanazoishi kukabiriwa na uchakavu.

Aidha askari hao wanalazimika kuishi chumba kimoja familia yeye mke na watoto jambo halikubaliki katika misingi ya haki za binadamu chumba kimoja kuisha familia nzima na kusababisha haki ya faragha kupotea katika maisha ya kila siku.

Katika hatua nyingine, Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu, Simai Mohamed Said, alisema kuwa wananchi wa Zanzibar wamekuwa wakipata shida wakati wa mvua kutokana na mji wa Zanzibar kukosekana kituo kikuu cha daladala pamoja na vituo vya gari za abiria na mabanda ya kujihifadhi kwa mvua na jua.

Alisema kuwa gari katika manispaa ya mji wa Zanzibar zimekuwa zikisimama ovyo na kuhatarisha uslama wa wananchi na mali zao.

Aliwambia Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) kuwa hivi sasa, Zanzibar kuna tatizo kubwa la baadhi ya wanaume kukosa nidhamu kwa kukojoa ovyo na kusababisha uchafuzi wa mazingira.

Alisema kutokana na kukosekana vyoo pamoja na kutunzwa vilivyokuwapo katika maeneo tofauti, Serikali imekuwa ikipoteza mapato mengi na kuna haja ya kufanyia kazi jambo hilo.

Chanzo: Nipashe

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s