Kibano Tume ya Maadili chatua Zanzibar

Rais wa Zanzibar akimpongeza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haroun Ali Seleiman mara baada ya kula kiapo cha utii
Rais wa Zanzibar akimpongeza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haroun Ali Seleiman mara baada ya kula kiapo cha utii

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imetangaza mpango wa kuwabana viongozi, wakiwemo Mawaziri, kutangaza mali wanazomiliki na madeni kwa kujaza fomu maalum Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Visiwani humo.

Mpango huo unanza mwaka huu wa Fedha na ulitangazwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haroun Ali Seleiman, wakati akiwasilisha makadirio na matumizi ya bajeti yake ya mwaka wa fedha 2016/2017.

Alisema serikali imeamua kuchukua hatua hiyo ikiwa ni juhudi za Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein katika kuimarisha misingi ya utawala bora kwa viongozi na watumizi wa umma katika kusimamia maadili ya viongozi.

Waziri Haroun alisema kuwa mpango huo ni utekelezaji wa sheria namba 4 ya mwaka 2015 inayowataka viongozi wa umma kuhakiki rasilimali wanazomiliki pamoja na madeni wakiwa katika nyadhifa za utumishi wa umma.

Alisema kuwa Dk. Shein ameunda Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma na kumteua aliyekuwa katibu Mku wa Wizara ya Sheria na katiba, Assah Ahmed Rashid kuwa mwenyekiti wa Tume hiyo.

“Mheshimiwa Spika viongozi wote wa umma na viongozi wa kisiasa wanaotajwa ndani ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 4 ya mwaka 2015, kuanzia mwaka huu wa fedha watawajibika kuwasilisha mbele ya tume fomu za tamko la mali na madeni yao,”alisema Waziri Haroun.

Alisema madhumuni makubwa ya kuundwa kwa tume hiyo kujenga misingi ya uwajibikaji na maadili pamoja na uwazi katika kusimamia sheria.

Alisema kuwa wananchi ndiyo wateja na waajiri wakuu wa watumishi wa umma, hivyo lazima kuwepo na misingi ya uwazi na uwajibikaji katika kuwatumikia wananchi wa Unguja na Pemba.

Chanzo: Nipashe

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s