Ukatili wa kijinsia: Wazazi kataeni kulipwa fidia

Afisa wa mradi wa TAMWA ofisi ya Zanzibar, Bi Grace Ngonyani
Afisa wa mradi wa TAMWA ofisi ya Zanzibar, Bi Grace Ngonyani

Wazazi nchini wametakiwa kuacha tabia ya kumaliza  kesi za ukatili wa kijinsia kifamilia na badala yake kuzifikisha katika vyombo  vya sheria ili  kuhakikisha zinapatiwa ufumbuzi na  hukumu za kisheria.

Hivi karibuni katika wilaya ya magharibi-Unguja kumezuka wimbi la vitendo vya ukatili wa kijinsia linalohusisha vipigo na  ubakaji  ambapo  baadhi ya familia zimekuwa zikimaliza kesi hizo kwa mazungumzo na kulipana fidia.

 Kwa mujibu wa  afisa  wa kushughulikia masuala ya ukatili wa kijinsia kutoka  TAMWA Bi Grace Ngonyani  ni kwamba ”jumla ya kesi sita   hazijaweza kufikishwa mahakani, na badala yake kuishia njiani bila hukumu kutokana na familia husika kukubali kupokea  fidia kwa lengo la kumaliza kesi hizo .

 Akitoa mfano “miongoni mwa familia za watoto waliobakwa  na kukubali suluhu kwa kulipwa fidia ni kesi iliyotokea fuoni meli sita, ambapo wazazi wa binti mwenye umri wa miaka 15 aliyedhalilisha kwa kukashifiwa na kjana wa umri wa miaka 34,  walikataa kufikisha kesi hiyo mahakani kwa ajili ya hukumu na badala yake kukubali fidia ya shilingi milioni tatu”.  

Mzazi  wa binti huyo aliyedhalilishwa kwa kukashifiwa, ameeleza kuwa wanahofu ya kupeleka kesi katika vituo vya sheria ili kusubiri mashtaka   kwani kesi nyingi za aina hyo huwa hazifikii mwisho na sheria kupindishwa hasa pale  watuhumiwa wanapokuwa na uwezo wa kifedha na kusababisha mtuhumiwa kushinda kesi,jambo ambalo Bi Fatma ameolina ni bora kupata kitu kuliko kukosa vyote.

 Aliongeza kwa kusema “ wazazi wengi wanapofika polisi hutaka walipwe fidia kwani endapo watakubali kesi kuendelea, inachukua muda mrefu na hatimae kufa bila kupatikana kwa  haki yoyote  na sababu mojawapo ni polisi  kuchelewesha kesi  kwa kigezo cha kutokamilika kwa uchunguzi wa kesi hizo”, alisema.

 Bi Grace alisisitiza kuwa hali hii inakatisha tamaa kwa  wanaharakati katika kufikia malengo ya kumaliza    aina zote  za udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto kataka jamii, kujua thamani yao na mustakabali  wa   maisha yao ya baadae.

Wazazi wahakikishe kuwa kesi zao zinafikishwa mahakamani na kupatiwa hukumu na sio kufuta  kwa madai ya kutokupata hukumu katika vyomba vya dola.

Vyombo  vya  kusimamia sheria   vihakikishe  kwamba kesi hizo zinapata hukumu na kwa wakati muafaka ili wazazi waweze kujenga imani na vyombo vya dola kwa  kuona haki inatendeka. Alimalizia Bi Grace.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s