Maalim Seif kikaangoni

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad

HALI ya upepo wa kisiasa Zanzibar, inatarajia kuchukua sura mpya leo wakati Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, atakapohojiwa na Jeshi la Polisi.

Maalim Seif anatarajiwa kuhojiwa leo kwa kile kiklichoelezwa na jeshi hilo kuwa ni juu ya masuala mbalimbali ya kiusalama. Awali alikuwa ahojiwe wiki iliyopita, lakini jeshi hilo liliahirisha kwa kile lilichoeleza kuwa ni sababu zilizo nje ya uwezo wao.

“Yale mahojiano yetu tuliyokuwa tumeyaahirisha Mei 26, sasa yatakuwa siku ya Jumanne (leo) saa nne asubuhi Makao makuu ya Jeshi la Polisi Kilimani,” alieleza Msangi katika barua hiyo.

Aidha, barua hiyo imemtaka Maalim Seif atakapofika makao makuu ya jeshi hilo kwa ajili kuhojiwa, aonane na Msangi.

Jeshi hilo limepanga kumhoji Maalim Seif kuhusiana na mambo mbalimbali ya kiusalama, yakiwamo matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea Zanzibar, baada ya uchaguzi wa marudio wa Machi 20, mwaka huu.

“Maalim Seif amekuwa akitoa matamko kadhaa ya kuwashawishi wananchi kupinga utawala wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyoko madarakani,” alisema Msangi wakati akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni.

Akizungumza na Nipashe, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CUF, Salum Bimani, alisema Maalim Seif amekubali wito huo na atahudhuria kama alivyotakiwa.

Alisema viongozi wa chama hicho, akiwamo mwanasheria wa Maalim Seif watamsindikiza kwa ajili ya kwenda kuhojiwa.

Bimani alisema CUF inalifuatilia kwa umakini suala hilo kutokana na kuwapo kwa taarifa zisizo rasmi kwamba kuna mpango wa kumweka ndani Maalim Seif baada ya kuhojiwa.

“Hatuamini kama Jeshi la Polisi litafanya hivyo na nilitake jeshi hilo lifanye kazi zake bila kufuata matakwa ya mtu au chama chochote cha siasa, ” alisema Bimani.

Hata hivyo, Bimani alisema baada ya kuhojiwa, wanatarajia kuwa Maalim Seif ataendelea na ziara zake za kichama na leo mchana atakuwa wilaya ya Kusini Unguja.

Chanzo: Nipashe

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s