Polisi yaahirisha kumhoji Maalim Seif

1613a-maalim252bseif

Jeshi la Polisi Zanzibar limeahirisha kumhoji Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad kwa sababu zilizoelezwa kuwa nje ya uwezo wake.

Katika barua yake kwa Maalim Seif iliyosainiwa na DCP Salum Msangi kwa niaba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar, haikutaja ni lini mahojiano hayo yatafanyika lakini imesema, “Tutakujulisha mapema siku ya mahojiano itakayofuata mara baada ya kukamilisha taratibu”.

Barua hiyo ya Mei 26 imenukuu barua ya awali ya Mei 22, 2016 iliyomuita mwanasiasa huyo makao makuu ya polisi Zanzibar kwa mahojiano kuhusu, “masuala mbalimbali yanayohusu ulinzi na usalama wa visiwa hivi.”

Kutokana na hatua hiyo, Maalim Seif aliyetarajiwa kuwasili saa 3 asubuhi Zanzibar kutoka Dar es Salaam kwa ajili ya kuhojiwa aliahirisha safari hiyo na atawasili Saa 10 za jioni kwa ajili ya maandalizi ya ziara yake ya kichama kuanzia kesho katika wilaya saba za Unguja.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s