Wapigwa marufuku kufuga ndevu Z’bar

beard chef

WIZARA ya Afya Zanzibar imewapiga marufuku wahudumu wa migahawa kutoa huduma kwa wateja wakiwa wamefuga ndevu.

Aidha, wizara hiyo pia imepiga marufuku wahudumu wenye kufuga sharubu au nywele.

Marufuku hizo zimeeelezwa katika mashariti 39 yaliyotolewa na Mkurugenzi wa Kinga, Dk. Mohamed Dahoma katika mkakati wa Wizara ya Afya katika kupambana na kipindupindu Zanzibar.

“Wafanyakzi wanatakiwa kupunguza nywele, masharubu, ndevu wakiwa katika maeneo yao ya kazi,” yameleeza mashariti hayo.

Kwa mujibu wa mashariti hayo, wafanyakazi wa migahawa wanatakiwa wasivae bangili au pete wakati wakipika pamoja na kucha zao ziwe fupi na safi.

Dk. Dahoma alisema wafanyakazi watatakiwa kupima afya zao kila baada ya miezi sita na lazima wawe wamepewa mafunzo ya huduma ya kwanza katika kupambana na majanga ya moto.

Mkurugenzi wa Kinga huyo alisema mpishi mkuu wa kila mgahawa ni lazima awe amepatiwa mafunzo katika taasisi inayotambuliwa na serikali na majengo ya migahawa lazima yawe na mwanga wa kutosha.

Aidha, chumba cha kulia kitatakiwa kiwe na ukubwa usiopungua futi 15 na upana futi 15.

Mkurugenzi huyo alisema kila mgahawa lazima uwe na bomba la kutolea moshi juu na liwe na urefu wa futi 10 pamoja na vyoo viwili kwa matumizi ya wanawake na wanaume.

Aidha, alisema kila mgahawa lazima uwe na kifaa maalum cha kugundua moto kabla ya kuleta madhara na vyumba viwili vya kubadilisha nguo, cha wanawake na wanaume.

Alisema kuwa mgahawa usitumike kama nyumba ya kuishi na lazima uwe unapitisha muangaza wa kutosha na lazima kuwepo na bomba maalum la kumwaga maji machafu.

Aidha, alisema wamiliki wa migahawa, imeelezwa ni lazima wazingatie usafi ikiwemo chakula kuhifadhiwa katika vyombo maalum bila ya kufikiwa na wadudu. Maji ya kunawa ni lazima yawe ya moto pamoja na wafanyakzi kuwa na sare.

Hata hivyo, wakizungumza na Nipashe mjini Zanzibar, baadhi ya wamiliki wa migahawa na maduka ya chipsi walisema mashariti yaliyotolewa utekelezaji wake utakuwa mgumu kutokana na mazingira ya nyumba za mji mkongwe.

Kassim Ali Humud, alisema kwa mashariti hayo migahawa mingi Zanzibar italazimika kufa na mamia ya watu watapoteza ajira.

Mmiliki wa mgahawa wa Darajani, Nassor Mohamed alisema mashariti yaliyotolewa na serikali ni mengi na yanahitaji gharama na muda wa kutosha badala ya kufanyika ghafla.

Mashariti hayo yametolewa huku migahawa na maduka ya chipsi ikiwa imefungwa kutokana na maradhi ya kipindupindua na kuathiri idadi kubwa ya wananchi wanaotegemea biashara katika maisha yao.

Chanzo: Nipashe

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s