Shajak akabidhi ofisi


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mhammed Aboud Mohammed kati kati akishuhudia utiaji saini wa makabidhiano ya Taasisi zilizopata uhamisho iliyotiwa na Katibu Mkuu Mstaafu wa iliyokuwa Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Dr. Omar Dadi Shajak kushoto na Katibu Mkuu Mpya wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Joseph Abdulla Meza.

Katibu Mkuu Mstaafu wa iliyokuwa Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Dr. Omar Dadi Shajak leo amekabidhi rasmi kwa Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar dhamana ya Taasisi zilizokuwa chini ya Ofisi hiyo.

Hafla hiyo fupi imefanyika katika Ofisi ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed ambae alikuwa shuhuda wa makabidhiano hayo yaliyoshirikisha pia baadhi ya watendaji wakuu wa Taasisi hizo.

Akimkabidhi majukumu hayo Katibu Mkuu Mpya wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Joseph Abdulla Meza, Dr. Omar Dadi Shajak alimtakia dhamana njema Katibu Mkuu huyo mpya katika usimamizi wa majukumu yake yaliyojumisha baadhi ya zile Taasisi zilizokuwa chini ya iliyokuwa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais.

Dr. Shajak alizijata Taasisi zilizokuwa chini ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ambazo zimehamishiwa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa ni pamoja na Idara ya Watu wenye ulemavu, Baraza la Watu wenye ulemavu, Tume ya Ukimwi pamoja na Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya Zanzibar.

Akipokea dhamana hiyo ya usimamizi wa Taasisi hizo Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Joseph Abdulla Meza ameahidi kuzisimamia kwa uadilifu Taasisi hizo kwa kuzingatia sheria, kanuzi za Utumishi Serikalini na Taratibu zote zilizowekwa na Serikali.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hivi karibuni imeweka muundo wa uwajibikaji uliozingatia mabadiliko kidogo katika baadhi ya Taasisi za Umma kufuatia uteuzi wa Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Wizara za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar pia imepewa dhamana ya kusimamia Tume ya Utumishi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar ambayo awali ilikuwa chini ya Ofisi ya Baraza hilo.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
27/4/2016.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s