Waandishi watakiwa kuondoka Dodoma

Edwin Soko

Tunaviomba vyombo vyote vya habari vya binafsi kususia kuandika habari za bunge hadi hapo litakapotengua utaratibu huo.

TAMKO LA OJADACT JUU YA WAANDISHI KUZUIWA KUINGIA BUNGENI KUFANYA COVERAGE

Ndugu waandishi wa Habari, wanaharakati na watanzania wote.

Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT). Tunalaani vikali kuzuiwa kwa Waandishi kuingia Bungeni kwa lengo la kufanya coverage ya vikao vya Bunge la kujadili mpango wa maendeleo ya miaka mitano na bajeti ya serikali.

OJADACT, hatukubaliani na utaratibu wa sasa wa kutumia idara ya habari na maelezo ya Bunge, kuwa ndio wenye jukumu la kukusanya taarifa na kuzigawa kwa waandishi.

Ni ukweli usiopingika kuwa, maamuzi hayo yana athari zifuatazo.

Kuminya uhuru wa haki ya kupata taarifa kwa wananchi km ilivyoainishwa kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano.wa.Tanzania ibara ya 18.

Kuminya uhuru wa vyombo vya habari, ambao umekuwa ukikosa haki ya msingi iliyokosekana kwenye Katiba.

MSIMAMO WETU.
1: Kwa kuwa Bunge halioni umuhimu wa waandishi Bungeni basi tunaviomba vyombo vyote vya habari vya binafsi kuwatoa waandishi wao bungeni.

Tunaviomba vyombo vyote vya habari vya binafsi kususia kuandika habari za bunge hadi hapo litakapotengua utaratibu huo.

Waziri mwenye dhamana ya habari afute kauli yake ya kejeli kuwa wanaopinga utaratibu huo eti waende Mahakamani.

Ahsanteni sana wanahabari kwa kuotokia wito wetu.

Edwin Soko
Mwenyekiti

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s