SMZ na Sweden watiliana saini mradi wa umeme


Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Nishati Ardhi na Makaazi Ali Khalil Mirza na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Multiconsult ya Norway Oyvi’nd Holtedahl wakipongezana mara baada ya kusaini Mradi wa kuimarisha huduma za umeme Zanzibar.

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar, imetiliana saini na Serikali ya Sweden makubaliano ya kuimarisha huduma za nishati ya umeme hapa nchini.

Katika hafla ya utiaji saini wa mradi huo, Zanzibar iliwakikishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Ardhi, Nishati na Makaazi Ali Khalil Mirza, wakati Makamu wa Rais Mtendaji wa Kampuni ya Multi Consult kutoka Norway Oyvind Holtedahl, alisaini kwa niaba ya Serikali ya Sweden.

Katika hafla hiyo iliyofanyika Makao makuu ya Wizara ya Maji, Ardhi, Nishati na Makaazi Katibu Mkuu Mirza, alisema kampuni ya Multi Cionsult ilishinda zabuni hiyo kati ya kampuni 12 zilizoomba kutekeleza mradi huo.

Alieleza kuwa mradi huo utakaochukua miaka mitatu na nusu hadi kukamilika kwake, utagharimu shilingi bilioni 12.7 za Kitanzania.

Amefahamisha kuwa, miongoni mwa matumizi ya fedha hizo, ni kuwapatia mafunzo wafanyakazi wa wizara hiyo ili kuwajengea uwezo wa kufanya tafiti ili wafanye kazi zao kwa ufanisi.

Mirza alieleza kuwa, lengo la Kampuni hiyo ni kusaidia katika kulijengea uwezo Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) pamoja na Idara zake kuhusu sera ya nishati ambayo ni muhimu kwa maenedeleo ya taifa.

Naye Mshauri Mwandamizi wa Kampuni ya Multi Consult ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwaamini kufanya kazi hiyo na ameahidi kuwa wataitekeleza kwa ufanisi mkubwa.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s