Mshauri wa Maalim Seif mbaroni

Mansoor Yussuf Himid ambaye ni Mshauri wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Hamad
Mansoor Yussuf Himid ambaye ni Mshauri wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Hamad

Salma Said, Zanzibar

Jeshi la Polisi linamshikilia Mansoor Yussuf Himid ambaye ni Mshauri wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Hamad.

Mansoor alipigiwa simu jana jioni na kuitwa na jeshi la polisi katika kituo cha Madema kwa ajili ya mahojiano akishutumiwa kuhusika na mambo mbali mbali ikiwemo suala la kuripuliwa kwa Maskani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kisonge Michenzani Mjini Unguja.

Akizungumza na Mwananchi, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam alithibitisha kukamatwa kwa Mansoor na kusema kwamba kutokana na hali ya matukio ya miripuko na mambo mengine wanahitaji kupata maelezo ya kina kabla ya kumuachia baada ya kupata ufafanuzi wa masuala hayo.

Alisema lengo la kumshikilia Mansoor sio kumkomoa bali ni kupata ufafanuzi na maelezo kwani hivi sasa kutokana na hali na matamshi ambayo huwa yanatolewa katika mitandao ya kijamii jeshi la polisi linafuatilia kwa kina na kuyachunguza.

“Ndio tunamshikilia Mansoor hapa polisi nani kwa sababu ya matukio mbali mbali ikiwemo hilo la kuripuliwa Kisonge, kwa hivyo tunataka maelezo na tukishapata maelezo yake tutaamua kama ni kumuachia au laa lakini kwa sasa tunamhitaji kwa kuisaidia polisi kwneye upelelezi” alisema Mkadam.

Wakati huo huo Kamanda huo alisema bado wanamshikilia Kaimu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa Chama Cha Wananchi (CUF) Hamad Masoud na watu wengine 38 ambao wanaisaidia polisi katika kufuatilia masuala tofauti yaliotokea hapa Zanzibar.

Hii ni mara ya pili kwa Mansoor kushikiliwa na jeshi la polisi ambapo mara ya kwanza aliwekwa kwa zaidi ya wiki moja kabla ya kupelekwa mahakamani.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s