Kigogo wa CUF na watu 42 mbaroni

Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Maasiliano ya Umma wa CUF Hamad Masoud Hamd, anayeshikiliwa na jeshi la polisi
Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Maasiliano ya Umma wa CUF Hamad Masoud Hamd, anayeshikiliwa na jeshi la polisi

Jeshi la polisi Zanzibar linawashikilia watu 42 kuhusiana na mripuko wa juzi usiku katika nyumba ya Kamishna wa polisi Hamdan Omar Makame.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za makamo makuu ya polisi Ziwani, Kamanda wa polisi wa mkoa wa mjini magharibi, Mkadam Khamis Makadam alisema kwamba hadi jana mchana watu 42 walikuwa ndani kwa ajili ya kuhojiwa na jeshi hilo.

Alisema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na bado kuna watu wanatafutwa kuhusiana na tukio hilo kabla hawajatoa taarifa kamili.

“Bado tunaendelea na uchunguzi wa jambo hili na tukishakamilisha tutatoa taarifa rasmi” alisema Kamanda Mkadam.

Wakati huo huo akiongea na waandishi wa habari Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Charle Kitwanga alithibitishwa kukamatwa kwa Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma wa Chama Cha Wananchi (CUF) Hamad Masoud.

“Polisi wanahitaji maelezo na ufafanuzi kutoka kwake kwa hivyo bado anaendelea kushikiliwa kwa kuhojiwa na polisi” alisema

Ingawa Waziri huyo hakubainisha mbele ya waandishi wa habari mambo gani ambayo yamesababisha kukamatwa na kuhojiwa kwa Kaimu huyo lakini siku ya Jumatatu, Hamad aliongea na waandishi wa habari na kuwaeleza kwamba hali ya kiuslama ni mbaya na haki za binaadamu zinavunjwa  hasa Kisiwani Pemba ambapo alishutumu jeshi la polisi kwa kupeleka silaha nzito na idadi kubwa ya askari kurandaranda mitaani kwa kuwabughudhi wananchi wa kisiwa humo.

Alisema kutokana na madhila hayo baadhi ya wananchi waliamua kukimbilia misituni na wengine kuanza kuhama na kuelekea Mombasa Kenya kunusuru maisha yao kama ilivyotokea mwaka 2000.

Akielezea kuhusuana na hali ya usalama Kisiwani Pemba, Kitwanga alisema suala la Pemba kwa bahati mbaya hazina ukweli wowote kwa kuwa kuna watu wanatoa taarifa ambazo sio sahihi kulingana na uhalisia wenyewe.

“Hali ya Pemba ni shuwari kabisa na pia nataka kusisitiza nikiwa kama waziri wa mambo ya ndnai sijapata taarifa yoyote rasmi kama kuna watu wanakimbilia nchi jirani lakini hata hilo la watu kukimbilia msituni inabidi tujiulize Pemba kuna msitu mkubwa wa watu kwenda kujificha? Haya mambo ni ya kuzusha watu waende wakajionee wenyewe” alisema Kitwanga.

Alisema hakuna dalili yoyote ya watu wanaokimbia watu kutoka Zanzibar na kukimbilia Tanzania Bara kutokana na idadi ya wasafiri kati ya bara na Zanzibar ni ile idadi ya kawaida.

Amesema kama kuna ongezeko lolote basin i kutokana na sherehe za Pasaka kukaribia na sio suala la kuongopa uchaguzi kama inavyoelezwa.

Waziri Kitwanga alisema yupo hapa Zanzibar ili kuhakikisha maandalizi yote ya uchaguzi wa marudio ya tanayotarajiwa kufanyika jumapili hususan kwenye upande wa usalama yanafanyika kama yalivyopangwa.

“Baadhi ya hivi vitisho vinavyoendelea tulivitegemea tunajua kama kuna watu hawataki uchaguzi na wanatumia mbinu mbali mbali ikiwemo huu miripuko kutisha watu. Wito wangu kwa watu wanaotaka kupiga kura wajitokeze kwa wingi na usalama wao upo” alisema waziri huyo.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s