Wazanzibari wako huru kupiga kura-Kificho

Mpiga kura akitumbukiza karatasi yake ya kura ndani ya sanduku la kura
Mpiga kura akitumbukiza karatasi yake ya kura ndani ya sanduku la kura

Zanzibar. Ikiwa zimebaki siku tano kufanyika kwa uchaguzi wa marudio wa Zanzibar, Spika  wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar,  Pandu Ameir Kificho amewataka viongozi wa siasa visiwani hapa kuacha kuwazuia wafuasi wao kupiga kura  Machi 20.

Wakati Kificho akisema hivyo, Kaimu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano kwa Umma wa CUF, Hamad Masoud Hamad  aliendelea kusisitiza kuwa chama hicho hakitarudi nyuma bali kitaendelea kudai haki.<

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Masoud alisema maamuzi ya Wazanzibari yaliyofanywa Oktoba 25 mwaka jana yatazingatiwa, kuheshimiwa na haki itatawala.

Kadhalika CUF walimuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania,  John Magufuli kuchukua dhamana katika suala hilo.

Taarifa ya CUF iliyotolewa kwa waandishi wa habari ilieleza kuwa chama hicho kiliwataka   Wazanzibari  kuwa wavumilivu katika hatua hizo za mwisho za kudai haki.

“CUF inawaomba wananchi wote kuendelea kuwa na subira na kuamini kuwa hizi ni hatua za mwisho za CCM kuelekea kufutika katika nyoyo za Wazanzibari, na kwamba wananchi wote  wavumilie  ili wafikie malengo yetu  ya muda mrefu ya kushika dola bila kumwaga damu,” alisema.

Kadhalika katika taarifa hiyo, CUF waliziomba Jumuiya za Kimataifa kuendelea kuitazama Zanzibar  kwa umakini wa hali ya juu na kufuatilia mwenendo na matukio yanayoashiria kuleta mvurugano ili baadaye ichukue hatua stahiki.

Kificho ahimiza upigaji kura

Akizungumza katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu wajibu wa kuripoti matukio ya Bunge, Kusini Unguja, Kificho alisema kura ni haki ya kila mwananchi.

“Wanasiasa hawana haki wala mamlaka ya kuwalazimisha wafuasi wao kususia uchaguzi kwani ni haki yao kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi,” alisema

Alisema kwa mujibu wa sheria ni haki ya kila mwananchi kuchagua na kuchaguliwa, hivyo wananchi waachwe ili wachague viongozi wao katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Chanzo: Mwananchi

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s