Maalim Seif azungumza na waandishi wa habari

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na waandishi wa habari katika hospitali ya Hindu Mandal Jijini Dar es Salaam kuelezea maendeleo ya afya yake. Amesema anaendelea vyema baada ya jana kuugua ghafla na kulazwa katika hospitali hiyo. Amewashukuru wananchi ndani na nje ya nchi kwa kuonesha mapenzi na mashirikiano makubwa. Anatarajiwa kutoka hospitalini hapo jioni hii
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na waandishi wa habari katika hospitali ya Hindu Mandal Jijini Dar es Salaam kuelezea maendeleo ya afya yake. Amesema anaendelea vyema baada ya jana kuugua ghafla na kulazwa hospitalini hapo. Amewashukuru wananchi ndani na nje ya nchi kwa kuonesha mapenzi na mashirikiano makubwa. Anatarajiwa kutoka hospitalini hapo jioni hii

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amezungumza na waandishi wa habari katika hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es Salaam, na kusema kuwa hali ya afya yake inaendelea vizuri.

Maalim Seif ametoa taarifa hiyo kufuatia kuugua ghafla jana asubuhi na kukimbizwa katika hospitali hiyo, ambapo alilazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Daktari wa Maalim Seif aliyeambatana naye akiwa Dar es Salaam Dkt. Omar Mohammed Suleiman amesema tatizo kubwa lililomkabili kiongozi huyo ni machofu aliyokuwa nayo baada ya kutokea safarini nchini India Ijumaa iliyopita.

Amesema alilazimika kulazwa hospitalini hapo ili kupata uangalizi wa karibu na kupumzika, na kwamba afya yake inaendelea vizuri na anatarajiwa kutolewa hospitalini hapo leo jioni.

Maalim Seif aliugua ghafla jana asubuhi akiwa safarini kuelekea  Dar es Salaam, hali iliyopelekea kukimbizwa hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es Salaam, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere.

hi3 hi2

Chanzo: OMKR

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s