Samia: Uchaguzi Zanzibar utafanyika salama, amani

Samia

Dar es Salaam. Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewahakikishia Watanzania na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuwa, uchaguzi wa marudio Zanzibar utafanyika na kumalizika kwa amani na utulivu.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Machi 20, baada ya ule wa Oktoba 25 mwaka jana kufutwa. Samia alisema hayo juzi alipokuwa akifungua semina ya uhusiano wa wabunge wa Afrika ya Mashariki.

Alisema Tanzania imekuwa kinara wa demokrasia kwa kufanya na kumaliza uchaguzi wake kwa hali ya amani na utulivu.

“Nawahakikishia Watanzania na nchi wanachama wa jumuiya yetu, Serikali itahakikisha uchaguzi wa marudio Zanzibar unafanyika na kumalizika kwa amani na utulivu kama ilivyokuwa uchaguzi ulliopita,” alisema.

Samia aliwataka wabunge wa Afrika Mashariki kujadili kwa kina na kuweka mikakati ya kuwa na sheria na taratibu bora, zitakazoziwezesha nchi wanachama kuwa na uchaguzi huru na haki.

Spika wa Bunge la EALA, Daniel Kidega alisema nia ya semina hiyo ni kuweka mifumo mizuri ili kuwezesha uchaguzi katika nchi hizo kuwa wa demokrasia, unaofuata utawala wa sheria na huru na haki.

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai alisema semina hiyo licha ya mambo mengine, itajadili umuhimu wa kuwa na uchaguzi huru kwa kuzingatia usalama na amani ili kuendeleza ustawi wa demokrasia.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

3 Replies to “Samia: Uchaguzi Zanzibar utafanyika salama, amani”

  1. Hawa viongozi wa Kiafrica wanafanya masihara na haki za wananchi wao…wana wafanya raia kuwa ni mando ndocha sasa ikiwa hawa wanao sema hivi ndio wasomi na viongozi wetu tunao watarajia watuongoze sisi wananchi tutakuwaje ? bado Africa ina kazi ya kupata uhuru wa kweli.

  2. We Samia we si tayari mumeshayapanga matokeo ya kura zenu batili hata uchaguzi wenu batili na wadhulma bado haujafanyika. Uchaguzi wenu wa 20/3/16 ni kilinge cha kuwaficha ukweli kondoo wenu wa CCM tu, ili yakija yakitendeka yaukweli mutafute kichaka cha kujifichia. We Samia we si mumeshampa Shein ailimia 51.80 na Seif 48 na Hamad Rashid abakie na asilimia zake zile zile . We Samia we , Si tayari mumeshapanga baada ya kumuapisha Mtanganyika Shein , ndipo Magufuli aje afanye suluhu baina ya Shein na Seif. Halafu muje mupitishe katiba yako na kuifilisi kabisa Zanzibar na baada ya hapo mumtawaze Nyerere kama mtakatifu kwa kuuondosha uislamu Zanzibar kwa kuwatumia waislam goigoi kama wewe dada yangu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s