Hili la Zanzibar lisiwe kama sikio la kufa halisiki dawa

Dk Ali Mohammed Shein
Dk Ali Mohammed Shein

Kuna misemo mingi katika kila lugha hususani lugha ya Kiswahili inayohimiza watu kuchukua tahadhari kabla ya hatari.

Misemo hii ni kama vile “Kinga ni bora kuliko tiba”, “Chukua tahadhari  kabla ya hatari” “asiye sikia la mkuu huvunjika guu”  ipo na mingine mingi  ya jinsi hii.

Yote hii ni katika jitihada za  wahenga wetu kujaribu kumtahadharisha mwanadamu kwamba kuna madhara makubwa sana kama kuna jambo au tatizo la kushughulikiwa leo likaachwa mpaka likawa kubwa sana na mara nyingi linakuja kumalizwa kwa gharama kubwa sana kwa vile linakuwa limeota usugu fulani.

Sote tunajua kwamba hata ugonjwa wa kawaida unaotibika kirahisi ukiachwa bila kutibiwa kwa wakati, huweza kuleta madhara makubwa  wakati mwingine hadi ya kifo.

Ugumu wa suala hili bila  shaka ni ukweli kuwa licha ya kwamba mgogoro huu ni wa kisiasa lakini chimbuko lake ni mgogoro wa kisheria uliotokana na tafsiri tofauti kati ya pande mbili zinazovutana.

Wakati upande wa CCM unaounga mkono kufutwa kwa matokeo ya  uchaguzi mkuu wa tarehe 25  na kisha kutangazwa kurudiwa kwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar kwa madai kwamba Tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) inayo mamlaka hayo kisheria na kwamba haipaswi kuingiliwa na mtu yeyeote.

Kwa upande mwingine ule wa  Cuf  unaopinga kufutwa kwa uchaguzi huo na kurudiwa kwake, kwa madai kwamba  aliyefuta uchaguzi ni mwenyekiti wa Tume ambaye kisheria hana mamlaka hayo labda tu kama amepata baraka za kikao halali cha Tume na kwahiyo madai yao ni kwamba hapakuwa na kikao halali cha Tume ya uchaguzi ya Zanzibar kilichokaa kutoa maamzi hayo.

Kwa bahati mbaya machafuko na vita vingi duniani huanza kwa sababu ya kutofautiana katika jambo dogo au kwa kupishana katika tafsiri ya jambo fulani.

Hata vita kuu ya kwanza ya dunia ilianza kwasababu upande moja katika mgogoro ( Austria – Hungary) ulikataa kuendelea na mazungumzo na upande mwingine  wa pili yaani Serbia.

Mgogoro ulianzia katika mauaji ya Archduke Ferdinand wa Austria- Hungary yaliyotekelezwa na vijana wa Kiserbia.

Hii ilisababisha Austria –Hungary kutoa masharti magumu kwa Serbia. Licha ya kuwa karibu masharti yote yalikuwa yamekubaliwa lakini sharti moja tu dogo hawakuafikiana na hivyo matokeo yake upande mmoja ukautangazia vita upande mwingine

Machafuko tunayoshuhudia kwa majirani zetu Burundi nayo pia yalianzia katika kutofautiana kwa pande mbili kuhusu tafsiri ya kisheria kuhusu maana ya misimu miwili ya uongozi ambapo upande wa rais Nkurunzinza ulishikiria msimamo kwamba kwa kuwa msimu wa kwanza wa utawala wake haukutokana na uchaguzi basi  hauwezi kuhesabika kama msimu unaotamkwa na katiba yao ya misimu miwili mtu kukoma kutawala

Upande wa pili ulishikiria msimamo kwamba rais Nkrunzinza alikuwa tayari ameisha ongoza misimu miwili inayotamkwa na katiba bila kujali kama ule wa kwanza hakuwa ameupata kupitia uchaguzi mkuu wa nchi hiyo. Matokeo yake pia yakawa ni machafuko tunyoyashuhudia leo.

Mifano hii miwili inasaidia kusisitiza pointi au hoja yangu kwamba  machafuko yanaweza kuanzia kwenye tofauti ya tafsiri ya jambo fulani ambalo laweza kuwa la kisheria au vinginevyo.

Pili mifano hii inasaidia kuonyesha kwamba pale pande mbili zilipoamua kusitisha au kuacha kabisa mazungumzo na upande mmoja kuchukua maamuzi ya kutekeleza matakwa yake, basi madhara makubwa ya machafuko yalitokea.

Chama tawala nchini Burundi kikiongozwa na Nkruzinza pia kiliacha  mazungumzo na kutangaza kibabe kuendelea na uchaguzi , matokeo yake nchi imeingia katika machafuko ambapo zaidi ya watu laki mbili wameishapoteza maisha na wengine wengi kuikimbia nchi yao na kuwa wakimbizi katika nchi jirani hasa Tanzania na haijulikani mwisho wake utakuwa nini.

Hapa tunajifunza kitu kingine muhimu kuhusu mgogoro wa Burundi. Mgogoro wa majirani zetu una chimbuko la tafsiri ya kisheria kama tulivyoona hapo mwanzo.

Tukidhani kwamba mgogoro wa kisiasa wenye ubishi juu ya tafsiri ya kishearia unaweza kumalizwa na mahakama tunajidanganya.  Kwa sababu Pale Burundi suala lao lilipelekwa mahakamani, mahakama ikatoa tafsiri ya kisheria kuhusu mgogoro ule kama ilivyoona inafaa.

Kisheria Nkruzinza alishinda na alipewa kibali kuendelea na uchaguzi. Lakini kama wote tunavyofahamu hilo halikuwa suruhisho la mgogoro huo.

Kwa hiyo tujifunze kwamba siyo kila mgogoro wa kisiasa unaweza kumalizwa na mahakama.

Sasa turudi hapa kwetu tuone mgogoro wa Zanzibar unavyoshughulikiwa. Hatua ya kwanza ilikuwa ni mazungumzo ya viongozi wa pande mbili kuu zinazo vutana CCM na CUF. Ingawa hatukupewa undani wa kilichoendelea lakini tunajua walishindwa kupata muafaka na hivyo mazungumzo yakakwama.

Kilichoendelea ni upande wa CCM kuendelea na kile wanachodhani ni sawa na wana uwezo wa kulazimisha kukifanyika ambacho ni kurudiwa kwa uchaguzi.

Upande wa pili katika mgogoro wanapinga vikali kurudiwa kwa uchaguzi  na wamejitoa hawatashiriki. Hadi hapo tayari tumeisha ingia katika matatizo makubwa.

Kama tulivyoona kwa wenzetu katika mifano ya hapo juu kwamba upande mmoja ukilazimisha kufanya unavyotaka ili hali wanamsuri , basi kinachofuata ni majanga. This is historical fact  (huu ni ukweli katika historia).

Katika hatua nyingine kwa nyakati tofauti viogozi wakuu wa pande zinazovutana walimtembelea rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John  Magufuli na kufanya mazungumzo naye na akawaahidi kutoa ushirikiano wake katika kusaidia kumaliza mgogoro huu.

Chanzo: Nipashe

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s