CUF yamtunishia misuli Jecha

mwenyekiti-wa-tume-ya-uchaguzi-zanzibar-zec-jecha-salim-jecha

Chama Cha Wananchi (CUF) kimeitaka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), kuhakikisha haitumii jina, alama wala picha ya mgombea yeyote wa chama hicho katika karatasi za kura za uchaguzi mkuu wa marudio utakaofanyika Februari 20, mwaka huu visiwani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano na Umma wa chama hicho, Hamad Masoud, alidai CUF inatambua kwamba Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha, anatekeleza maagizo ya chama chake, Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alisema CUF inawataka wananchi wote wa Zanzibar, Tanzania na jumuiya ya kimataifa kutambua kwamba Jecha ametoa taarifa ya uongo ili kuendeleza upotoshaji alioanzisha kwa tamko lake la kufuta uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana na kuamuru kurudiwa uchaguzi huo.

Alisema CUF haitashiriki katika uchaguzi huo wa Machi 20, mwaka huu na kuichia CCM iendelee kujitangazia ushindi wa urais, viti vyote 54 vya uwakilishi na viti vyote 111 vya udiwani.

Alisema CUF kitaendelea kusimamia maamuzi yake waliyafanya kuwa hawatashiriki uchaguzi huo wa marudio katika nafasi zote.

Wakati huhuo, chama hicho, kimelitaka Jeshi la Polisi Zanzibar, iwapo kweli lina kesi dhidi ya mwanaharakati wa CUF, Eddy Riyami, limfikishe mahakamani haraka ili hatua za kisheria zifuate mkondo wake na iwapo hawana kesi wamwachie huru.

Riyami anashikiliwa na Jeshi la Polisi tangu  juzi kwa tuhuma za kumtukana na kumkashifu Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, pamoja na Jecha.

Chanzo: Nipashe

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s