Wanawake CUF kupinga uchaguzi Zanzibar kwa maandamano, polisi yasema marufuku

CUF Wanawake

Dar es Salaam. Jumuiya ya Wanawake ya Chama cha Wananchi (CUF) imepanga kufanya maandamano kuelekea kwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan yenye lengo la kuunga mkono uamuzi wa uongozi wa chama hicho kutoshiriki uchaguzi wa marudio kisiwani Zanzibar.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro amezuia maandamano hayo kwa sababu mbili. Alisema uchaguzi huo uko chini ya ZEC na mipaka yake inajulikana na pili, alisema njia sahihi kama wanataka kupinga ni kwenda mahakamani.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Severena Mwijage alisema maandamano hayo yatafanyika Jumatatu ijayo na yataanzia katika ofisi za CUF zilizopo Buguruni.

Mwijage ambaye pia ni mbunge wa viti maalumu kupitia chama hicho alisema jumuiya hiyo imeamua kuandamana kwenda kwa Makamu wa Rais kwa kuwa wanaamini ndiye pekee mwenye sifa za kuuelewa ujumbe wao.

Alizitaja sifa hizo ni pamoja na kuwa Mzanzibari hivyo, kwa kuwa tatizo hilo lipo Zanzibar, yupo katika nafasi nzuri ya kuwaelewa pamoja na ujumbe watakaompelekea. “Sababu nyingine ya kuamua kumpelekea ujumbe wetu Mama Samia ni kwa kuwa yeye ni mama na mwanamke mwenzetu.

Endapo hali ya amani iliyopo Zanzibar itavunjika watakaoathirika kwa kiasi kikubwa ni wanawake na watoto hivyo tunajua yeye akiwa mama ataupokea na kuufanyia kazi ujumbe wetu,” alisema Mwijage.

Alisema tayari wameomba kibali cha kufanya maandamano hayo Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na kusema wanaamini kwamba watapata ushirikiano mkubwa kwa kuzingatia kuwa maandamano hayo ni ya amani.

Alisema maandamano hayo yatapita barabara ya Uhuru, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Karume, Kariakoo, Mnazi Mmoja, Kituo cha Polisi Kati, Barabara ya Sokoine, Bandari, Mahakama Kuu ya Ardhi hadi Ofisi ya Makamu wa Rais

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s