Misingi ya haki ituelekeze kutenda haki Zanzibar

Salma Said, Mwananchi
Tokea kuibuka kwa mgogoro wa kisiasa Zanzibar kufuatia kufutwa kwa uchaguzi na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, kumekuwa na mitazamo na mapendekezo tofauti ya kumaliza mgogoro huo.

Wengi wanaopendekeza kutatuliwa kwa mgogoro au mkwamo wa kisiasa uliopo Zanzibar uliotokana na uchaguzi  wanahofia kutokea uvunjifu wa amani pindi mgogoro huu usipotatuliwa. Hili ni kweli na lina umuhimu wake kabisa.

Tayari wanasiasa mbali mbali, viongozi wa dini tofauti, wasomi na hata wale ambao ni wafuatiliaji wa masuala ya kisiasa na chaguzi katika nchi mbali mbali wameona kwamba huenda uchaguzi ukirudiwa kunaweza kuleta matatizo na kuvunjika kwa amani na kuleta mgawanyiko wa wananchi wa wananchi wa Unguja na Pemba na Zanzibar kurudi katika siasa za chuki na hasama kama ilivyokuwa kipindi cha utawala wa Dk Salmin Amour Juma ambaye kwa kiasi kikubwa joto la kisiasa lilikuwa kubwa mno.

Hata hivyo ni vyema twende mbele zaidi. Inawezekana kabisa wengine wakadhani kuwa hili halitotokezea hasa wale waliopo madarakani wanao amini nguvu za dola walizozijenga na wanaamini zitawalinda hata wakifanya nini. Hili si sahihi hata kidogo.

Siku zote maneno mawili yamekuwa yakidanganya sana; nguvu, uwezo (power) na udhaifu (weekness). Tunaweza kudhani baadhi yetu tuna nguvu sana za kijeshi nk lakini isiwe hivyo. Tunaweza kuamini kuwa nguvu hizo zinaweza kutulinda vyovyote iwavyo kumbe sio hivyo.

Kwa upande mwengine tunaweza kuona wengine ni dhaifu; hawana jeshi na hata silaha moja lakini kumbe si dhaifu. Uwezo na udhaifu usitudanganye.

Katika dunia ya leo matumizi ya nguvu vyovyote iwavyo havionyeshi kufanikiwa bali huzidisha upinzani kila kukicha. Hili limekuwa likijihidhirisha hata hapa Zanzibar.

Tukirejea hali ilivyokuwa mwaka 1995 na leo ni tofauti. Upinzani Zanzibar umekuwa sana licha ya matumizi makubwa ya nguvu yanayofanywa na vyombo vya dola. Mifano iko mingi duniani ya hali kama hii. Ndio mana mwanaharakati na mpigania haki wa Kimarekani, Dr. Martin Luther King alikuwa anapenda kuongea maneno haya

“The Stronger than all armies is an idea whose time has come” Kwa msingi huo ni muhimu kusimama katika misingi ya haki siku zote ambayo ndio njia pekee ya kumaliza migogoro yetu na hata mgogoro huu wa Zanzibar.

Viongozi wetu wawe ni kielelezo cha kutenda haki ili sisi wananchi tujifunze kutoka kwa viongozi hao kutenda haki.

Binafsi mimi nilifurahi sana nilipomsikia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli alipokuwa akihutubia uwanja wa Taifa siku alipokuwa anaapishwa alisema hivi: kuwa “Tumuweke Mungu mbele” huku akirejea kauli hiyo mara kadhaa.

Nilifurahi kwa sababu kwa kumuweka Mungu mbele yeye na viongozi wenzake watakuwa wanaongoza kwa misingi ya haki, uadilifu, uwajibikaji, sheria na mambo mengine muhimu kama hayo.

Na sisi wananchi pia tungefuata misingi hiyo pia na hivyo kuwa na Taifa linalopenda haki, uadilifu na uwajibikaji ambayo ndio misingi muhimu ya kuwa na amani na utulivu wa kweli katika taifa loloe duniani, kwani bila ya misingi hiyo tutajidanganya tu na kurudi nyuma.

Kunaweza kusiwe na vita lakini kukawa hakuna amani hata kidogo. Watu watakuwa wanalalamika, kutukana na kujenga chuki dhidi ya serikali yao, kukakosekana uwajibikaji ufanisi wa kazi ukakosekana na hata ile ari ya kulitumikia taifa na wafanyakazi wa serikali kukosa ari ya kufanya kazi huku wananchi wakiwa kwenye taharuki na kuvunjika moyo.

Binaadamu hatakiwi kuamini katika nguvu tu kuwa ndio kigezo cha kutotenda haki. Uwezo mkubwa tulionao na udhaifu mkubwa tunaouona wengine wanao visitudanganye na kuacha kutenda haki. Tusimame na haki kama kweli tunataka kumuweka Mungu mbele kama alivyosema Dk Magufuli.

Mgogoro wa Zanzibar unaweza kumalizwa kwa kuzingatia misingi ya haki. Tutende haki tuwe na Taifa litakaloishi kwa amani, umoja na mshikamano wa kweli. Tukiumaliza mgogoro huu kwa kuzingatia haki na maridhiano ya kweli, tutaweza kuwafanya watu wa itikadi tofauti

Chanzo: Mwananchi

One Reply to “Misingi ya haki ituelekeze kutenda haki Zanzibar”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s