Mabalozi wakomalia maridhiano kabla ya uchaguzi Zanzibar

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akihutubia wakati  akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika Mchapalo wa Mwaka Mpya kwa Mabalozi na Wawakilishi wa Taasisi mbalimbali za Kimtaifa maarufu kama "Sherry Party" Ikulu jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akihutubia wakati akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika Mchapalo wa Mwaka Mpya kwa Mabalozi na Wawakilishi wa Taasisi mbalimbali za Kimtaifa maarufu kama “Sherry Party” Ikulu jijini Dar es Salaam jana

Dar es Salaam. Jumuiya ya mabalozi nchini imeendelea kushikilia msimamo wao wa kuitaka Serikali kutafuta suluhu shirikishi ya mgogoro wa kisiasa Zanzibar, licha ya Serikali kusema kuna nafasi ya mazungumzo ya namna ya kuboresha uchaguzi wa marudio.

Kaimu kiongozi wa mabalozi hao, Edzai Chimonyo alisema jana kuwa jumuiya hiyo inaiomba Serikali itumie busara kutafuta suluhu ya kudumu kumaliza mvutano unaoendelea visiwani humo ili Wazanzibari waendelee kuishi kwa amani. “Kuhusu suala la Zanzibar, ni matumaini yetu kuwa kupitia busara na ushauri wako suluhu inayokubalika pande zote mbili itapatikana,” alisema Chimonyo ambaye pia ni balozi wa Zimbabwe nchini.

Mabalozi na Wawakilishi wa Taasisi mbalimbali za Kimtaifa wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akihutubia wakati  akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika Mchapalo wa Mwaka Mpya  maarufu kama "Sherry Party" Ikulu jijini Dar es Salaam
Mabalozi na Wawakilishi wa Taasisi mbalimbali za Kimtaifa wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akihutubia wakati akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika Mchapalo wa Mwaka Mpya maarufu kama “Sherry Party” Ikulu jijini Dar es Salaam jana

“Wazanzibari wameungana na kuacha tofauti zao na tunaamini wataendelea kufanya hivyo ili kudumisha umoja na amani.” Alisema jumuiya hiyo inaamini pia kuwa Serikali itakamilisha mchakato wa Katiba mpya uliokuwa umeanzishwa na Serikali iliyopita ambao ulikwama kutokana na kutokamilika mapema kwa Daftari la Wapigakura.

Kuhusu mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar, Wazoro wa Mambo ya Nje, Dk Augustine Mahiga alisema pamoja na Zanzibar kuwa ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ina mfumo wake wa kisiasa, utamaduni, Serikali, Katiba na tume huru ya uchaguzi.

Alisema baada ya mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Jecha Salim Jecha kufuta uchaguzi kwa sababu ya kukiukwa kwa sheria na kanuni za uchaguzi, kulianzishwa mazungumzo baina ya pande zinazohusika lakini muafaka haukufikiwa na mbadala ukawa kurudia uchaguzi.

Dk Mahiga aliiomba jumuiya ya kimataifa kuunga mkono uamuzi huo wa kurudia uchaguzi akisisitiza kuwa bado kuna nafasi ya wadau na pande zinazohusika kufanya mazungumzo ya kuboresha uchaguzi huo.

mahi8

Alisema Serikali yake itaendelea kushirikiana na jumuiya ya kimataifa katika masuala mbalimbali

Chanzo: Mwananchi

One Reply to “Mabalozi wakomalia maridhiano kabla ya uchaguzi Zanzibar”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s